Hivi Sungura anataga Mayai au Anazaa? Nimeulizwa na binti aliyetoka kufanya Usaili wa ualimu hivi karibuni

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Leo mida ya mchana wife akiwa anatoka kanisani alikuwa ameongozana na binti muhitimu wa chuo cha ualimu.
Hapa nyumbani nimefuga sungura wapo watatu nimenunua hivi karibuni baada ya madogo kuwapeleka kwa mfugaji mwenzangu wakawapenda sana nikaamua kuwanunulia .Muda ule walinikuta nahangaika kuwaingiza badani baada ya kutoka bandani.

Alipowaona alifurahi sana na baada ya kukamata sungura mmoja alitamani na yeye amshike nikawa nimempa
Swali alilo niuliza liliniacha mdomo wazi "HIVI SUNGURA ANATAGA MAYAI AU ANAZAA?" Nikijua labda sijasikia vizuri akarudia tena swali lile lile. Nikamjibu sungura anazaa kama wanavyo zaa paka na mbuzi au nguruwe anazaa na hatagi mayai

Nikamuuliza kwani shuleni mlifundishwa kuwa anataga ? akajibu hata hajui yeye siku zote anajua sungura anataga mayai kama bata au kuku!!

Ni kitu kidogo sana hiki lakini mimi kimeniacha na maswali mengi sana.Tazamia huyu apate ajira tofauti na a e i o u alizo karirishwa chuoni ana vitu gani vingine vya kufundisha watoto wetu kama viumbe wa kawaida kabisa kama sungura hajui kama anazaa.Mtu kafika level ya chuo na bado hajui.

Nimejifunza elimu yetu pia ni kimeo sana hivyo uwepo ulazima wa kwenda kujifunza kwa vitendo kwa wafugaji walio karibu na shule au wafugaji waombwe waende shuleni wakafundishe kwa vitendo hasa wakiulizwa maswali.Na kumbuka kipindi chetu kulikuwa na somo stadi za kazi moja ya mada ilikuwa ufugaji mwalimu wetu(rip)alitupeleka kwa mfugaji wa kuku,ng'ombe na mbuzi.Tuliuliza maswali mengi na yote tulijibiwa japo mfugaji yule alikuwa anafuga kienyeji tu.

Mfugaji au mkulima ni rahisi sana kujibu swali na kueleweka maana yeye ana fanya kazi kwa vitendo.Haya mabadiriko ya mitaala yazingatie sana elimu kwa vitendo na iwe kipaumbele.

Mbona kwenye kipindi cha dini wachungaji na mashekh huwa wanakuja kufundisha itashindikana vipi sisi wakulima na wafugaji kwenda kuwafundisha watoto/wadogo zetu ? Naimani tukipewa muda hakuna atakaye kataa kuwafundisha watoto wetu kwa vitendo.

Mwalimu hata kama umesomea masomo ya sanaa pekee yake ndo usijue kama sungura ni mnyama na sifa ya mnyama ni kuzaa?
 
Anazaa
 
Umeamua kuwavua nguo walimu sasa
 
Huyo asifaulu hiyo interview atafanya vijana wetu wa kayumba kuwa vilaza walioshindikana.
 
Kuna vitu vidogo vodogo binadamu huwa hatuoni umuhimu kuvijua au hatujawahi kuvizingatia, hata wewe utakuwa na kaujinga flani
Ni kweli lakini siyo kwa Namna hii kabisa bona haya tumefundishwa kabisa kuanzia primana Olevel mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…