Kwa jinsi kauchumi chetu kalivyo HAKUNA FAIDA YOYOTE NI KUPOTEZA PESA ZA WALIPA KODI NA MUDA
ila indirectly familia za wanaoenda zinafaidika saana kwani wahusika wanalipwa perdiem, pesa za usafiri na mengineyo
Mkuu, katika "economy at large", hule mkutano haukuwa na faida, yaani multiplication effects zake katika uchumi wa taifa ni cheche tu...
ILA, kuna watu binafsi walifaidika, kivipi;
(1) kuna tenda mbalimbali katika uendeshaji wa ule mkutano, watu walipiga ela, haijulikani gharama halisi ya ile shughuli, watu wamepiga.
(2) kupitia ule mkutano, kuna miradi mingi imeanzishwa au itaanzishwa kupitia ule mradi, sasa kuna watu watakuwa wameiweka mifukoni ile miradi, watakuwa wamejipanga namna ya kula kwenye hiyo miradi....
Hii ndio Tz yetu, siku zinaenda...
Hakuna cha maana zaidi ya ile miti mithili ya minazi iliyopanda katika barabara ya Sam nujoma,faida nyingine(-ve) kipindi cha mkutano nilikuwa nachelewa shule daily kisa foleni