Bwana/bi Adabet,
Kwa namna ulivyouliza swali lako umewatia kichefuchefu wanasheria waliomo humu jamvini,
ambao bila kujali hasara wanazopata hutoa ushauri na elimu ya bure humu kuhusiana na mambo
mbalimbali ya kisheria.Ndiyo maana umeona wamebaki kimya bila kukujibu kwani mtu mwenye akili kubishana na mwehu ni
vigumu mtu mwingine mwenye busara akatofautisha kati ya mwehu na mzima kiakili.
Kuwa Mwanasheria siyo jambo rahisi ambalo mtu aliyefeli analiweza, mtu aliyefeli
anazo dalili kama zako za kupayuka, tena hatari sana unapopayuka kupitia maandishi. Wanasheria ni watu
wanaoheshimiana sana. Taaluma hii inayo miiko yake kama ilivyo kwa madaktari, ndiyo maana huwezi kusikia
wala kuona tangazo la biashara la mwanasheria kutangaza huduma yake kuwa ni bora kupita ya mwingine.
Endapo ulihitaji kuelimishwa ungeuliza swali kistaarabu ili ujibiwe.
Tanzania haina utaratibu wa ku-classfy murder offence into degrees, ie first degree murder, second...,etc.
kila mtu aliyeshiriki kuua hata kama katika hatua ya kula njama hushitakiwa kama principal offender.
kuhusu kutakasa fedha ipo sheria ya Anti money laundering Act. Endapo unazo habari za watuhumiwa wa aina hii unaweza kuzifikisha PCCB au kwa DCI tena kwa siri bila mtu yeyote kukufahamu, ndipo uone kama hatashughulikiwa. Tafakari uchukue hatua!!
Watu hufikishwa mahakamani lakini ni haki ya mtuhumiwa kupata dhamana, ndiyo maana unawaona mitaani.
Kuhusu kesi uliyoitaja ni jambo la kawaida mtu kutokupatikana na hatia kutokana na mtizamo wa jaji aliyeisikiliza kesi,
lakini ushahidi huohuo ambao jaji wa awali aliukataa waweza kukubaliwa kwenye rufani.
Sheria ni Bahari pana sana kuweza kuogelea hapa.
Karibu tena wakati mwingine ukiwa unalo tatizo...usiwanyime wengine fursa ya kufaidika humu kwa kuwatukana wataalamu wetu.