Hivi Tanzania na Africa hatuna uhusiano na Latin America?

Hivi Tanzania na Africa hatuna uhusiano na Latin America?

BigBro

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
3,585
Reaction score
11,601
Huwa najiuliza marais wa Africa ikiwemo Tanzania hatuna uhusiano na nchi za Latin America?(America Kusini). Nakumbuka Jakaya Kikwete aliwahi tembelea Brazil lakini sio nchi kama Paraguay, Colombia, Argentina, Ecuador, Venezuela, Chile na nyinginezo.

Na pia marais wa huko ni kama hawana time na Africa. Tatizo nini? Ubalozi tunao pale Brazil ambako nimewahi kufika.

Nilifika Colombia wanaijua South Africa zaidi, Tanzania wengi wao hawaijui angalau Kenya na Rwanda wanaijua. Marekani ndio kama katawala magari yao mengi yanatoka USA kama ilivyo Mashariki ya kati kwa nchi ya Lebanon kukuta Toyota ni nadra sana. Shida ni nini?
 
Sasa wabongo wakiishi huko kifuatacho si unakijuwa mkuu

Mahusiano hatuna kivile na nchi za huko labda brazil,sema wapo wabongo wanaoishi peru, Argentina
Brazil hapo ndy usisemeee

Ova
Katika nchi zote za Latin America Argentina haina uhuni mwingi. Pale Bogota Colombia hapana aisee, siku 14 nilizokaa pale ilikuwa kama mwaka. Africa hakuna wahuni na watemi wanaigiza tu
 
Tuwashobokee wananini wakati wao ni Kama sisi tu si Bora India ana adi nuclear na viwanda vya magari wao kule Wana Nini chaku tu impress walau kidogo Brazil Yuko Brics ataeleweka hao wengine ni halima naomba chumvi kama Afrika
 
Mimi nadhani Hakuna fursa za kutosha huko ndio maana raia wa huko wanakimbilia USA,kiasi Kwamba mpaka Trump akatakaga kujenga ukuta mpakani lakini pia umbali wa kijiografia kutoka huku inaweza pia ikawa sababu ya waafrika kutoshoboka nako
 
Rula Inancio da Silva rais wa brazil aliwahi kuja tanzani na akawa mgeni rasmi katika ufunguzi wa maonyesho ya kimataifa ya biashara za nje maarufu kama maonesho ya sabasaba jijini dar es salaam. Hizo nchi za amerika ya kusini ubalozi wa tanzania ulioko brazil utakuwa unashughulika nazo. Kule amerika ya kati nchini cuba kutakuwa na ubalozi wa tanzania ambao nao utakuwa unashughulika na nchi za eneo hilo. Kuna nchi nyingi tu tanzania haina ubalozi nazo ila balozi za tanzania zilizo jirani na nchi zitakuwa zinashughulikia mambo ya kidiplomasia kama kuna umuhimu. Hata bara la asia kuna nchi nyingi hazina ubalozi wa tanzania
 
Latin yote ubalozi niliona Brazil tu, hata kwenda Colombia tulisaidiwa Brazil kwa kila kitu. Ila lile bara hawajui chochote zaidi ya Marekani. Ukiwa black unaongea English wanajua wewe ni wa Marekani. Wanaiabudu Marekani mno. Halafu lile bara asilimia 99.9 ni wakatoliki, nilichoka
 
Tatizo nchi za huko nyingi hasa colombia uhuni wa kuuza ngada ndo unasumbua sana, ukienda kwa nchi zenye ustaarabu wakaiona passport yako inaonesha ulikuwa na safari za huko wanakuchunguza kweli kweli.
 
vipi huko kuna waislam? Na huko mexco waafrika wapo? Kule kweli ni ukatoliki mtupu ndio maana lugha ya kilatini inatumika sana katika mambo ya kikatoliki
 
Tatizo nchi za huko nyingi hasa colombia uhuni wa kuuza ngada ndo unasumbua sana, ukienda kwa nchi zenye ustaarabu wakaiona passport yako inaonesha ulikuwa na safari za huko wanakuchunguza kweli kweli.
Uzuri tulikuwa kwenye delegates, hatukupata shida, tulirudi kupitia South Africa saa 11 hewani
 
Safi sana mkuu, ukiachana na makando yao hivi ni vitu vipi uliona wametuzidi kwa mbali ambavyo tunapaswa tujifunze?
Zile nchi Marekani ndo kila kitu. Mimi nazaliwa Keko niliiona Shell pale mnazi mmoja. Kule Shell ndo kila kitu kwenye vituo vya mafuta. Wametuzidi miundo mbinu sisi bado sana. Ila zile muvi za kihuni za Marekani kule ndo maisha hasili
 
Mexico wanaongea Spain, lakini haipo Latin America wao ni Central Amerika. Sikuona msikiti Colombia
vipi kuhusu makaburi ya kifahari ya wauza mihadarati huko mexico ni kweli yapo na yanalindwa vikali na magenge ya wauza mihadarati? Kama yapo mbona yanaweza kugeuzwa ni sehemu ya makumbusho na utalii kwa jinsi yalivyojengwa kwa gharama kubwa?
 
Sikuwa Mexico ile sio Latin America ingawa wanaongea Spain. Ila Latin America kuna wanawake wazuri sana na wana matako kama Africa
 
Huwa najiuliza marais wa Africa ikiwemo Tanzania hatuna uhusiano na nchi za Latin America?(America Kusini). Nakumbuka Jakaya Kikwete aliwahi tembelea Brazil lakini sio nchi kama Paraguay, Colombia, Argentina, Ecuador, Venezuela, Chile na nyinginezo.

Na pia marais wa huko ni kama hawana time na Africa. Tatizo nini? Ubalozi tunao pale Brazil ambako nimewahi kufika.

Nilifika Colombia wanaijua South Africa zaidi, Tanzania wengi wao hawaijui angalau Kenya na Rwanda wanaijua. Marekani ndio kama katawala magari yao mengi yanatoka USA kama ilivyo Mashariki ya kati kwa nchi ya Lebanon kukuta Toyota ni nadra sana. Shida ni nini?
Kama Paraguay ina vifaru vya kijeshi 22 sisi tunavyo 42 tuitembelee tugundue nini?

Waje watutembelee wao tuwafundishe na kuiba kura
 
Back
Top Bottom