sblandes
JF-Expert Member
- Apr 25, 2010
- 6,980
- 4,992
Shida ndio hiyo,Kwa wananchi walio wengi itakuwa ngumu kupuuzia miradi anayofanya Magufuli.Sasa wataweka kitu gani tuwaelewe wakati sisi tunaona yaliyofanywa kwa macho yetu?
Labda katika wabunge,Chadema inaweza ikapata wabunge wasiozidi 30,na sababu kubwa ,watu walio wanachama na wasio wanachama wamepoteza imani ya wabunge wa upinzani hasa Chadema kukimbilia CCM.
Chadema itumie uchaguzi mkuu kujenga chama tokea ngazi ya shina,iachane kusajiri waroho wa msimu wa kuvuna pale panapotangazwa uchaguzi.