Hivi TBC sio Free to Air Tena?

Hivi TBC sio Free to Air Tena?

Ile dhana ya fair competition inakuwa haipo. Wao wanaendeshwa kwa pesa ya Serikali. Wenzako wanajiendesha kwa pesa zao ikiwemo wanazozipata kwa matangazo ya biashara.
Ndio maana ingebidi TBC hasionyeshe Matangazo wala asichague Programs hata zile ambazo sio Commercially Viable ila zina mchango kwa Taifa aweze kuzionyesha...

Kwahio kama hawa wengine wanaona hawapati fungu kipindi hiki cha World Cup basi TBC awagawie kipato chochote cha kipindi hiki na sio vinginevyo
 
Pole mkuu watu wengi washakubali utalalamika tu bure
Kwamba huku ni kulalamika, au kuhoji matumizi ya kodi zetu na kupindishwa kwa Sheria !???

Alafu watu wanalalamikia watu na Kampuni zao eti wasiwapangie bei ya Bundles wakati huku wanachokilipia hawakipati !!!, Wanasahau kwamba Kodi zetu through Ruzuku ndio zinaendesha hii Kampuni...,

Wanashidwa kuelewa impact ya hili sio kila mtu ana pesa za kulipia kuweza kuangalia huu mpira na ni vijana wangapi huenda wangekuwa motivated kucheza mpira ili wawe kama fulani kwenye Kombe la Dunia ?
 
Mkuu, mimi bado sijaelewa unacholalamika ni nini?
Hilo ni Swali kwamba hii sio FTA tena ?
Issue ni kuwa haipo kwenye category ya FTA, au ipo lakini wameiondoa sababu ya WC au kuna visimbusi haipo tena?

Naomba fafanua.
Sasa kama haipo kwenye VISIMBUSI mpaka ulipie hivyo VISIMBUSI hio ni FTA ya wapi tena ?

Kumbuka hapa nimekuja na maswali hili nipate majibu sijaja na conclusion...
 
TBC FM ndo free kwani huna redio na mpira wanarusha TBC FM
Ukitaka Tv bas nunua kifurushi acha kupenda vya bure
 
TBC FM ndo free kwani huna redio na mpira wanarusha TBC FM
Ukitaka Tv bas nunua kifurushi acha kupenda vya bure
Naam ndio nayosema hayo hata mtu hujui bure ni nini na nini unakilipia; Hapo ulipo unalipia TBC wanayopewa kama Ruzuku; Pia TBC ni Free to Air hata contract na mechi walizopewa ni sababu ya kuwa TV ya Taifa ambayo ni Free to Air..

Kwahio mkuu TBC ni Free to Air na visimbusi kama Continental; Startimes na vingine kama hivyo kulingana na leseni yao wanatakiwa kuonyesha channels zote za Free to Air hata kama mtu hana Kifurushi..., hao wauza madish kina DSTV ni tofuati na huenda hii Sheria haiwabani...
 
Na hapa ndio watanzania Tuna-Fail; Haujui kwamba Kodi yako inatumika kuendesha TBC; Hence hata kama hauangalii ni kwamba Pesa yako inatumika ndivyo sivyo...

Na hii ndio inapelekea walamba Asali kuchonga Mzinga...,

Enjoy maisha bana kodi gan iyo unayochangia ad uanze kulalamika ivyo sasa kodi ulipe ww na bado ufe kwa presure na stress kibao kisa kodi
 
Naomba kujuzwa hii TBC inayoendeshwa kwa Ruzuku zetu ni lini imebadilika kutokuwa Free to Air ?

Kama ni issue za Word Cup huu ndio utapeli kwamba watu wanunue vifurushi ili waone mama anaupiga mwingi ?, Huyu Nape na hawa TCRA wameshindwa Kazi ? au watafuatilia na kuleta majibu baada ya Kombe la Dunia Kuisha, na hapo ndio itarudi kuwa Free to Air ?

Sina neno kama sio Free to Air, basi iache kuchukua Ruzuku, sio vema Ruzuku wachukue alafu kwenye vingamuzi vingine isifanye kazi; Kama vipi wawalipe hivyo Vingamuzi ili wawaonyeshe kwenye hii la World Cup
Tbc kuna baadhi ya frequency ni free to air, na kuna baadhi sio mfano ukiingiza frequency za azamu hata TBC haitakubali kufunguka kwa kuwa wanazi encript zitumike kwa vingamuzi vya kampuni husika kwa sasa kama unataka free to air ni lazima uwe na dish kubwa na utumie channel za west kupata tbc
 
Enjoy maisha bana kodi gan iyo unayochangia ad uanze kulalamika ivyo sasa kodi ulipe ww na bado ufe kwa presure na stress kibao kisa kodi
Wewe kama umeamua kukaa kimya ni Prerogative yako..., ila kumwambia mwingine akae kimya nadhani ni kuwa na Upeo Mfupi..., Ila nakukumbusha ni Jukumu lako kuongea iwapo kodi yako haifanyi kazi yake...

Huenda upo Qatar unaangalia mpira Live ila sio kila Mtoto / Kijana; ailyepo Tanzania anauwezo wa kununua Kifurushi ila kuangalia huu Mpira hata Fifa wameweka urahisi ili mtoto huyo aweze kuona, sasa wengine kutumia hii fursa kwa mavuno hence kumkosesha kijana kama huyu hii furaha sio Poa...
 
Tbc kuna baadhi ya frequency ni free to air, na kuna baadhi sio mfano ukiingiza frequency za azamu hata TBC haitakubali kufunguka kwa kuwa wanazi encript zitumike kwa vingamuzi vya kampuni husika kwa sasa kama unataka free to air ni lazima uwe na dish kubwa na utumie channel za west kupata tbc
Nadhani AZAM watakuwa na a Case sababu wenyewe leseni yao ya hizo Dish ni kwamba inabidi uweke pesa ili uweze kuangalia channels na hizo za bure hata wasipoweka siwezi kuwalaumu sana...

Ila hawa kina Continetal na wenzao leseni zao za hizo decoder ni lazima waonyeshe hizi free to air tofauti na hapo wanakiuka leseni zao
 
Back
Top Bottom