Hivi TCRA imewashindwa kabisa hawa watu wanaotuma SMS za kitapeli au kuna nini kinachoendelea?

Braza Kede

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2012
Posts
3,840
Reaction score
6,844
eti wakuu

Kunani hapa?

Mbona bado hizi meseji za ajabuajabu zinaendelea kutumwa licha ya mabiti yanayopigwa kila mara na hawa jamaa wa TCRA?

Kwanini hawafungiwi hawa watu?

Screenshot_20250214-144634_Messages.jpg
 
Hata Mimi wamenitumia Upumbavu huu,tuna hiyo sms kwenye namba 15040.
mimi naona kama mfumo wa kupata hizi namba umekuwa rahisi sana ndomaana mtu anaweza akafanya ujinga akijua akishtukiwa anaenda kusajili namba nyingine mpya.

ilibidi wakaze kwenye usajili wa hizi namba isiwe mchekea kama hivi.

halafu wachukue majina yote matatu ya mtu akizingua tu unakata usajili wake mazima kwa mitandao yote. hii michezo ingeisha.
 
Hiyo kazi ni ngumu sana. Tanzania wengi bado washamba hata waliofika chuo wenye degree.

Wanaosajili laini ndio wanafanya uhuni wa kusajili laini kwa taarifa za mtu, watu hawajua hata kuangalia namba zilizosajiliwa na NIDA yake.

It will takes time, mana kuna human error nyingi na sio technical
 
Wakalitazame!
 
apo shida ipo kwenye izo kampuni ya simu maana hata kama taarifa zinaingizwa na wale vijana wa mitaani mwisho wa siku kampuni ndo wanasajili izo taarifa.

sasa kama taarifa zake hazieleweki au hazifanani na nida yake unamsajili vipi mtu huyo?
 
eti wakuu

Kunani hapa?

Mbona bado hizi meseji za ajabuajabu zinaendelea kutumwa licha ya mabiti yanayopigwa kila mara na hawa jamaa wa TCRA?

Kwanini hawafungiwi hawa watu?

View attachment 3236559
Kumbuka ajira yao inategemea uwepo wa matapeli hao, wakiwamaliza(uwezo wanao) hawatakuwa na kazi ya kufanya.
Siku wahalifu wote nchini wakiokoka nchi haitakalika, polisi wataandamana, mahakimu na mawakili nao pia, askari magereza pia wataandamana, wapishi wa magereza na madereva wa polisi, mahakama na magereza nao wataleta balaa. Kwa jumla baadhi ya ajira zinategemea uhalifu wakiwemo na viongozi wa dini wanaoishi kwa sadaka zetu.
 
Na kusema ukweli hao matapeli wanafanikiwa kwani kuna mmoja hawa wanaotuma ujumbe wa kusafisha nyota na kutoa utajiri
Alifanikiwa kupata hausigeli aliyetaka kusafisha nyota alianza nae taratibu mpaka yule hausigeli kumkaribisha nyumbani mabosi wakiwa kazini.....Tapeli alifanikiwa kuondoka na pesa ya kutosha baada ya kufanikiwa kuingia chumba cha mwenye nyumba, kupekua kabati na kufanikiwa kukutana na bahasha iliyohifadhiwa kiasi cha dola 3000
 
daah akasafisha nyota kiukwelikweli
 
Back
Top Bottom