Ndyali
JF-Expert Member
- Nov 24, 2011
- 1,678
- 971
Akili yangu inajua kuwa tangu awamu ya tano ingie madarakani, Bunge si la Wananchi tena ! Kwani tayari lime- compromise. Bunge kulazimishwa lisiwe live kwa Wananchi ni Bunge la Wananchi? Bunge ku- edit speech za wabunge ndipo zirushwe hewani kwa Wananchi ni Bunge la Wananchi? Bunge la Ndugai limekuwa la double standard sana kwa wabunge wa upinzani. Kwanza kwa kumtumia Lipumba lilianza kuwasambaratisha wabunge halali wa CUF, lakini pia lilikithiri kuwasimamisha kuingia Bungeni hao uliowaita wawakilishi wa Wananchi kutoka CHADEMA kwa makosa ambayo hayakustahili kuwasimamisha kuingia Bungeni wabunge hao.