Hivi TRA kwa sasa hawatangazi makusanyo kila mwezi?

Mimi sijui zinanipita habari hizi maana sijaona muda tra wakitangaza makusanyo ile kila mwezi kama zamani au utaratibu umebadilika
Fedha za Kutangazwa hazipo tena kwakuwa hivi sasa kila Mtanzania anakusanya za Kwake na Kujitangazia Wenyewe tulizozikusanya Mioyoni Mwetu.
 
Haya mtoa mada mwenye kiherehere na viherehere woote kwa ujumla wenu mmetangaziwa huku "angalieni mjiridhishe ili muifurahishe mioyo yenu mpate na kamisheni zenu za kukaguakagua"
SISI WENGINE TUNAANGALIA TU.
Shule zinajengwa?👍
Barabara zinajengwa?👍
Huduma mahospitali zipo?
👍
Miundombinu mingine?👍
Miradi viporo inaendelezwa👍
 
Acha porojo na ujinga mwingi
 
Fedha za Kutangazwa hazipo tena kwakuwa hivi sasa kila Mtanzania anakusanya za Kwake na Kujitangazia Wenyewe tulizozikusanya Mioyoni Mwetu.
Mkuu sasa hivi wanatangaza mikopo tu waliyokopa kwa wazungu.
 
Unataka tuwe tunatangaziwa mapato kanjanja kama ya wakati ule!,Tunachotaka ni ukusanyaji ufanyike na mambo yaendelee kama sasa miradi yote inasonga mbele mabarabara yanajengwa mishahara inalipwa what's else!
::Ukitangaziwa itakusaidia nini?
Haustahili kuwa jukwaa hili, hivi hakuna majukwaa ya watoto?
 
Kwani ikitangazwa wewe unapata asara gani na kwanin unaumia wanaposema kutangazwa, mwanafunzi anayepata zero mara kwa mara hawezi kufurahia kutangazwa kwa matokeo ya mtihani waliofanya. Punguza ujinga, hizo ni hela zetu lazma tujue kiasi tulichochanga kwa ujumla wake na sisi ndio wenye mamlaka ya kuwaamuru watangaze au wasitangaze.Ila nchi hii mijitu mijinga ni mingi sana.
 
Mimi sijui zinanipita habari hizi maana sijaona muda TRA wakitangaza makusanyo ile kila mwezi kama zamani au utaratibu umebadilika?
kumbe miezi mitatu ya mwanzo ilikuwa bado haijaisha naona wameshatangaza makusanyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…