Hivi tukiamua kuachana na shilingi tukatumia dolar itakuwaje?

Shilingi yetu ipo vizuri ila tatizo hatuna export kubwa kuliko import, that's why Kenya wanatuzidi kwa sababu wanaimport bidhaa zetu kwao na wanaexport kwenda nje kwa thamani kubwa zaidi.
Serikali inapoinject fedha katika mzunguko huwa haifikii walengwa au dhumuni husika.
 
Sorry, yawezekana una point, lakin unaweza kunielezea like unamsimulia mtoto wa darasa la kwanza!.
 
Kwema wakuu.

Maisha yetu yanakuwa magumu, fedha yetu inakosa thamani. Hivi kama taifa likatelekeza shilingi na kuanza kutumia dolar ya Marekani tataathirika ama kufaidika na nini?
Fedha za nchi nyingi ambazo zimeshuka sana thamani, zimefanya dollarization, yaani wanatumia fedha isisyo yao.

Suala hili mbali na uzuri wako linakuwa na shida kwenye uchumi wa nchi ambapo nguvu ya benki ya taifa husika inaathiriwa. Ambapo hapo hamtaweza kuwa na sera ya fedha ya kwenu, mtakuwa mnafuata sera ya fedha ya wenye hela yao.

Nchi inapopoteza kitu kiuchumi kinaitwa 'Seigniorage power' ni tatizo kubwa sana. So ni vizuri kubadili currency lakini sio kutumia fedha ya mtu mwingine.

Kama utasoma ripoti za BoT kila mwezi huwa wanaangalia kiwango cha dollarization ili kuona kama kuna haja ya kuweka sawa sera ya fedha za kigeni.
 
Technically Tanzania tunatatizo la balance of trade yaan import>export
hii ndio hasa sababu demand ya pesa yetu ipo chini koz hatuuzi bidhaa nyingi nje Ila tunanunua bidhaa nyingi nje
Sera babaishi za kodi ndio zinatufikisha hapa
 
Imagine unanunua mkate kisha unalipa USD 100 chenji inakuwaje πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€!
 
Kwema wakuu.

Maisha yetu yanakuwa magumu, fedha yetu inakosa thamani. Hivi kama taifa likatelekeza shilingi na kuanza kutumia dolar ya Marekani tataathirika ama kufaidika na nini?
Umeuliza swali zuri sana kijana na sijaiona mtu yeyote alieweza kulijibu.
Nachokiona hapo ni kila mtu anajaribu kuelezea anachokijua kwenye masuala ya uchumi Ila wanashindwa kujibu swali.
Jibu swali kama vile ungejibu ukiwa kwenye chumba cha mtihani acheni blah blah hit the target.
 

Sehem pekee ya kupigia bao ni kwenye natural resources tu ila tushafeli hatuna wachumi hapa tz pale BOT wanawaza asali tu
 
Be straight, tukitumia US dollar Badala ya Tsh madhara ni yepi na faida ni ipi kama ipo?
 
Elimu yako tafadhari, kabla sijakujibu
Mi nadhani wewe ndie unaepaswa kutufahamisha kiwango cha elimu yako!
Sidhani kama jibu la swali hili linahitaji mtoa jibu kujua elimu ya muuliza swali.
 
Kuwa na thamani kubwa ya pesa haimanishi mna uchumi imara, Zambia wana Export Shaba pekee, Kuwa na pesa yenye thamani kubwa kuna madhala kuliko faida
yes in kweli kabisa solo la dunia linaushindan mkubwa kuongeza thaman ya currency in sawa na kipandisha bei ya kile unachokiuza sokon sio rahisi koz solo la dunia halipo free kuna competition so kuwa na curreny yenye low value inasababisha tuuze bidhaa zetu ghafi kwa bei ndogo yenye kukubalika sokon
 
mkuu unaishi kwa mazoea,uthamani wa local currency na ikiwa ni sarafu ya kibiashara faida ni kubwa sana,mfano bei ya petrol/diesel kwa soko la ndani, sarafu ya nchi husika ni moja ya sababu kuwa bei itapanda au kushuka, kwa muda wa miezi miwili sasa bei ya bidhaa hii kwa zambia, Botswana, namibia, SA,imekua inashuka kwetu hapa ni politics tu, zambia wana export sio shaka pekee!!wameshaanza pia to export agricultural products, idadi ya raia hawazidi 22M, sisi almost 60M
Kuwa na thamani kubwa ya pesa haimanishi mna uchumi imara, Zambia wana Export Shaba pekee, Kuwa na pesa yenye thamani kubwa kuna madhala kuliko
 
ninaweza kukuunga mkono. mfano parachichi letu ni bora lakini linapitia kenya then abroad . unafikiri tunakwama wapi sisi kwenye issue za kutafuta masoko ili tuwe na high exportations??
 
Wewe ndio hujaelimika.

mtoa mada kaweka uzi ili aeleweshwe wewe unamsimanga

Kwani hazitumiki? Hotelini ,Kwenye maduka makubwa ,kwenye mashirika ya ndege ,kwenye makampui ya utalii zinatumika.........1 usd = 2300Tsh ,ukienda sehemu yoyote kama una usd wewe piga mahesabu kisha utoe equivalent in USD.
 
Kufanya mapinduzi ya viwanda ili kuweza kuexport bidhaa ni gharama na inachukua mda na technologia pia, kumbuka pia ushindani ni mkubwa kutoka kwa wale mabwenyenye wa uzalishaji/viwanda mfano China na USA. Njia nyepesi ni kuwekeza kwenye natural resources na bidhaa za kilimo! Mbona nchi za Asia wanatumia mafuta na gesi kukuza dhamani ya pesa yao? Kwanini na sisi tusitumie madini yetu na gesi yetu kupaisha Tsh. Yetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…