Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndege atoke Amerika ya kusaini atuletee magugu maji?Miaka ya 90 mwishoni yaliibuka kwa wingi sana ikawa habari kubwa ziwa Victoria. yameota tena. Kumbuka kila mmea una mbegu yake inayoweza kusambazwa na ndege upepo, mkondo wa maji n.k.
Magugu maji yameharibu sana mwonekano wa ziwa nyanza.Magugu maji hutokea kutokana na kuzidi Kwa virutubisho vya nitrogen na phosphorus ndani ya maji (eutrophication), chanzo Cha virutubisho hivi ni kutokana na vinyesi vya wanyama (akiwemo binadamu) kuingizwa majini (Sewage system directed into water bodies).
Ukiangalia Kwa upande wa ziwa Victoria, makazi kuzunguka ziwa Hilo hayana mfumo mzuri wa vyoo. Hivyo wakati wa mvua inasemekana flushing hufanyika kuelekezwa ziwani. Hivyo kuongeza virutubisho (nutrients content), na kupelekea magugu maji ndani ya maji.
Faida za magugumaji Kwa samaki.
1.Husaidia kujificha Kwa baadhi ya samaki pindi wanapowindwa
2.Hutoa kivuli na sehemu za kupumzika Kwa samaki.
3.Baadhi ya samaki(Egg beater) hutumia magugumaji kutengeneza viota vya kutagia mayai.
4.Ni sehemu mhimu ya kukuzia vitoto vya samaki (Nursery grounds)
Hasara za magugumaji.
1.Hupelekea upungufu wa oksijeni (Hypoxic and anoxic condition) kutokana na ushindani wa matumizi,
2.Hupunguza uangavu wa maji(water clarity) na kupelekea kupungua kiwango Cha mwanga jua kufikia viumbe maji.
3.Hupunguza uzuri wa mazingira ya majini na huduma zingine (water beauty and amenity)
Mkuu, unafahamu kuwa kuna mienendo ya ndege, kuwa wakati wa baridi kali ulaya wanahamia bara la Africa?Ndege atoke Amerika ya kusaini atuletee magugu maji?
Mfano ndege yupi aliyetoka America ya kusinni akafika ziwa nyanza?Mkuu, unafahamu kuwa kuna mienendo ya ndege, kuwa wakati wa baridi kali ulaya wanahamia bara la Africa?
Ndivyo ilivyo mkuu,Magugu maji yameharibu sana mwonekano wa ziwa nyanza.
Hii ya kusema, chanzo Cha magugu ni maji tiririka Toka vyooni, umeitoa wapi?
Nyasa na Tanganyika hakuna vyoo na kemikali zinazotiririka ziwani?Ndivyo ilivyo mkuu,
Ziwa Nyasa na Tanganyika hamna vitu kama hivyo, kutokana na mazingira kuzunguka maziwa hayo.
Hayo yapo lakini ziwa Victoria pamezidi sanaNyasa na Tanganyika hakuna vyoo na kemikali zinazotiririka ziwani?
Tutafiti zaidi, nadhani Kuna zaidi ya hapo!!
Una Elimu ya darasani kiwango kipi?Wewe ni MPUMBAVU, unapewa majibu sahihi kuhusu chanzo cha magugu maji wewe umekazania kuwa yamepandikizwa na watu.
Nenda mto Kagera uone ulivyozungukwa na magugu maji kwenye kingo zake.Ziwa Victoria magugu maji yamekuwepo tangu miaka na miaka na sio jambo jipya kama unavyotaka kuaminisha watu hapa.
Nimezaliwa na kukulia kwenye visiwa vya ziwa Victoria so najua ninachokisema.
Project za watu hizo.Salaam, Shalom!!
Nilipokuwa katika ziara ya Utalii wa ndani, nimekumbana na kero hii ya magugu maji ziwa Viktoria. Ziwa NYANZA lilikua ziwa la kuvutia sana.
Wataalam wasema, haya magugu ziwa NYANZA hayakuwepo miaka ya nyuma, ni mradi umetokea miaka ya hivi karibuni,
Serikali na wanavijiji kuzunguka ziwa NYANZA wamekuwa wakihangaika kutokomeza magugu hayo.
Magugu hayo yamechangia kupunguza kuzaliana Kwa Samaki ziwa NYANZA Kwa kadri siku zinavyoenda. Historia ya Kutokea magugu hayo ziwa NYANZA inasemaje na hatua zipi zinachukuliwa kukabiiana na uharibifu huo wa kutengeneza?
Swali: Ni nani waliyehusika kupandikiza magugu ziwa NYANZA?
Na wakibainika, ni Bora washtakiwe, walipe fidia, na wayaondoe Kwa gharama zao, ni akina nani hao?
Karibuni 🙏
Picha ya ziwa nyanza na magugu yake!!Uzi bila picha ni batili
Jadili mada uliyoileta.Huu upumbavu wa kukwepesha mada wafanyie wapumbavu wenzio.Una Elimu ya darasani kiwango kipi?
Samahani lakini!!
Ni vizuri nikajua kiwango Cha Elimu Yako,Jadili mada uliyoileta.Huu upumbavu wa kukwepesha mada wafanyie wapumbavu wenzio.
Yanazuia Samaki kufikia mapango Yao ya kutagia mayai.Mimi nilijua magugu maji ndio kuongeza kasi ya kuzaliana samaki.
Ok, hiyo ni nature msimtafute mchawi