Hivi tumeshindwa kushawishi TOYOTA ilete kiwanda Tanzania?

Hivi tumeshindwa kushawishi TOYOTA ilete kiwanda Tanzania?

Kwa takwimu zisizo Rasmi 75% ya magari yote Tanzania ni aina ya TOYOTA. Suala lililobaki ni kuchukua takwimu kutoka TRA ndani ya miaka 10 ni magari mangapi aina ya TOYOTA yaliingia Tanzania (mapya na yaliyotumika) jumlisha na mengine yalikuwepo ambayo bado yapo barabarani + yale yaliyoagizwa kupitia TZ kwa sababu nalo ni soko.

Twende kuongea nao tukiwa na DATA na sio maneno matupu. Toyota na viwanda vingine vipo kiashara hivyo visababu vya kujibia mitihani haviwashawishi kwani vipo hata kwenye Nchi nyingine.

Tukikosa kiwanda rasmi tunaweza kupata hata centre kubwa ya spea OG za TOYOTA kwa bei poa. Tukiendelea Kulala Usingizi, hiyo fursa itaenda kwa wenzetu walio aggressive kwenye fursa.
Bahati mbaya Toyota hawatengenezi gari mitumba hivyo hawawezi kuja.
 
Wazo zuri sana kwa spea sawa ila kiwanda kizalishe magari ya 0 KM hayatanunuliwa hapa kama bado hadi sasa tunaagiza magari used tena ya mwaka 2002
Yatapungua bei kama yatakuwa yanatengenezwa hapa na ITAKUWA ni kitu kinachowezekana kabisa kwa mtu wa KAWAIDA kununua GARI brand new. TATIZO labda ije iwe KUNA WATU AMBAO huwa wanapitishia madeal yao kwenye uagizaji wa magari kutoka nje ya nchi, HICHO kiwanda hakitakuja kuwepo HATA SIKU moja
 
Purchasing power ya Watanzania ni ndogo mno.

Gari nyingi mpya bei yake ni kubwa.

Hatuna malighafi
Hatuna viwanda vya malighafi
Hatuna uwezo wa kununua mapya tunanunua used tu ingawa tunasema tumenunua gari jipya[emoji3][emoji3]
 
Kuna tetesi walitaka kuweka assembly plant maeneo ilipokuwa external service ya RTD, wenye roho mbaya wakavuruga huo mpango
 
Serikali ya ccm inajiona yenyewe ndiyo ina haki ya kununua na kuendesha magari mapya! Halafu wananchi wanatakiwa kununua used from Japan!
Mkuu kama mfuko unakuruhusu unaenda tu TOYOTA pale,au CMC nk
Unajifyatulia machine 0 km
Magari ya mitumba si yameanza kuingia miaka ya mwisho 80 tu
Ila kabla ya hapo magari yalikuwa yanayotumika ni mapya tu

Ova
 
Uwezo wetu wa kununua gari jipya ni mdogo sana. magari mengi tunayoendesha ni used na Toyota haina records za Tanzania kununu Toyota. Ingekuwa magari yote tunayoendesha yangenunuliwa yakiwa mapya hicho kiwanda kingekuwa hapa siku nyingi.
Mbona watu wanavimba nayo fresh tu hayo hayo magari used.
 
Tatizo letu sio lingine bali ni kuwa na watu wanaojituma na waamini wanaojali kazi zao kwa nia moja

Kuunganisha magari sio kazi ngumu kama kuna wataalamu ila je vifaa vitabaki salama?

Tulikuwa na Scania na kazi ilikuwa nzuri zamani kwa nidhamu ya hali ya juu kabla shetani hajapiga kambi rasmi Bongo

Nilileta pikipiki mpya na kuajiri vijana waziunganishe ila nikawa nazikagua kila wanapomaliza kazi na mimi nikiwa hapo
Unaona washeli (washer na nuts kama Tatu unauliza na hizi mbona hamkufunga?

Jibu la kisen@ unaambiwa eti hizo ni za ziada
Na zingine hazijafungwa mpaka mwisho
Sasa kwa mafundi wa hivi kweli ajali zitaisha nyumbani?

Utakuta hata magari yanapofanyiwa services huwa wanalipua lipua tu na mwisho police wanasema ooh break mara gari limeacha njia

Maamuzi anatoa police asiejua ajali imesababishwa na nini maana gari halipelekwi kwenda kufanyiwa uchunguzi wa kina kujua tatizo haswa ni nini mpaka gari limeanguka?
 
Kwa takwimu zisizo Rasmi 75% ya magari yote Tanzania ni aina ya TOYOTA. Suala lililobaki ni kuchukua takwimu kutoka TRA ndani ya miaka 10 ni magari mangapi aina ya TOYOTA yaliingia Tanzania (mapya na yaliyotumika) jumlisha na mengine yalikuwepo ambayo bado yapo barabarani + yale yaliyoagizwa kupitia TZ kwa sababu nalo ni soko.

Twende kuongea nao tukiwa na DATA na sio maneno matupu. Toyota na viwanda vingine vipo kiashara hivyo visababu vya kujibia mitihani haviwashawishi kwani vipo hata kwenye Nchi nyingine.

Tukikosa kiwanda rasmi tunaweza kupata hata centre kubwa ya spea OG za TOYOTA kwa bei poa. Tukiendelea Kulala Usingizi, hiyo fursa itaenda kwa wenzetu walio aggressive kwenye fursa.
Kati ya hii 75%, asilimia ngapi hununuliwa mapya? Watz hatuna uwezo wa kifedha wa kununua gari kutoka kiwandani, uchumi hauruhusu.
 
Purchasing power ya Watanzania ni ndogo mno.

Gari nyingi mpya bei yake ni kubwa.

Hatuna malighafi
Hatuna viwanda vya malighafi
Tatizo ni uwezo wa kununua, malighafi wangezileta wenyewe.
 
Ni kweli serikali iko sahihi kabisa kwani tuliumbwa na miguu ili iweje? Jamani tuacheni kupenda na kuendekeza anasa.
Kama wako sahihi mbona wananunua V8 mpya kabisa, tena za kumwaga? Si wangetembea kwa miguu, au wao hawakuumbwa na miguu?
 
Kama wako sahihi mbona wananunua V8 mpya kabisa, tena za kumwaga? Si wangetembea kwa miguu, au wao hawakuumbwa na miguu?
Tembea kwa miguu wewee acha porojo miingii na mbofumbofu jamvin
 
Back
Top Bottom