Wana jf, hivi kwa sasa tunahitaji Katiba mpya kwanza au tunahitaji kufanyika kwa mijadala rasmi juu ya Katiba mpya. Nimeulilza hivi kwa sababu kuna watu wanataka tudai Katiba Mpya bila ya kujali kuwa hakujawahi kuwepo kwa mjadala rasmi juu ya Katiba mpya. Tusipoiona haja ya kufanyika kwa mijadala rasmi juu ya Katiba, watatokea wajanja ambao watapeleka Mswada Bungeni wa kutaka Katiba mpya na ukakubaliwa na ikaundwa Katiba nyingine hata kama ni kwa jina tu. Lakini tukidai mjadala rasmi, sio rahisi kuchezewa shele. Nawasilisha