Hivi tunapaswa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa au kulia kwa uchungu?

Hivi tunapaswa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa au kulia kwa uchungu?

ommytk

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Posts
520
Reaction score
1,143
Kumekuwa na utamaduni wa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa kwa kila namna na kila utaratibu je hii ni sahihi au tulipaswa tusikitike na kulia kwa uchungu maana siku zako za kuishi dunia zinaisha au hii ikoje wajuzi wa mambo mje hapa
 
Kumekuwa na utamaduni wa kushehekea siku zetu za kuzaliwa kwa kila namna na kila utaratibu je hii ni sahihi au tulipaswa tusikitike na kulia kwa uchungu maana siku zako za kuishi dunia zinaisha au hii ikoje wajuzi wa mambo mje hapa
Watu wa Mungu mna matata😃
 
Sasa mjuba na ndevu zako na meno 32 inafika siku ya kuzaliwa unaanza kulia chozi kabisa? Seriously?

Ebana em acha masikhara, kula maisha furahia kuwepo duniani, ila tu usisahau kumkumbuka Mungu, tambua ana maksudi yake kukuleta hapa duniani..

We live once & die!
 
Kumekuwa na utamaduni wa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa kwa kila namna na kila utaratibu je hii ni sahihi au tulipaswa tusikitike na kulia kwa uchungu maana siku zako za kuishi dunia zinaisha au hii ikoje wajuzi wa mambo mje hapa
Yote mawili yanatuhusu. Furaha ya kuona umeifikisha miaka hiyo, kisha huzuni kuwa kati ya miaka unayo kadiria kuishi mwingine umepungua.
 
Unatakiwa kusikitika maana siku za kuishi ndo zinaenda hizo, ohooooo....
 
Kumekuwa na utamaduni wa kusherehekea siku zetu za kuzaliwa kwa kila namna na kila utaratibu je hii ni sahihi au tulipaswa tusikitike na kulia kwa uchungu maana siku zako za kuishi dunia zinaisha au hii ikoje wajuzi wa mambo mje hapa
Hiyo hoja yako Ina mitazamo miwili; mtazamo wa kwanza ni wa kidunia, ni kweli wapo baadhi hawafurahii umri kusonga, na hii ni mara nyingi inatokana na mwenendo wa kimaisha (burudani, srarehe, anasa, raha, nk). Huyu atataka kila siku awe hivyohivyo, yaani asizeeke, ili aendelee kufanya hayo mambo.

Mtazamo wa pili ni wa kiroho; hapa mtu anawaza na kujibidisha (kujiandaa) na maisha yanayofuata, yaani maisha ya milele. Huyu kwake birth day haina maana yoyote. Kwa umri aliokuwa nao, wowote ule (awe kijana au mzee), anachojali kwa wakati huo ni moyo wake kuwa msafi (hapa moyo upe nafasi ya nafsi). Mtu wa aina hii kifo kwake sio issue, maana yuko tayari muda wote. Kwa hiyo kwa habari ya kujali umri (birth days), tuangalie mitazamo hiyo mawili.
 
Lazima ufurahi bila kujali miaka iliyobaki. Kumbuka kuna watu walitamani kufikia umri huo. Wengine wanafia tumboni, wengine wanatupwa kwenye condom.
 
Back
Top Bottom