Hivi TV za Mewe ni nzuri kweli?

Mewe? Piga chini broh, lasivyo utakuja kujilaumu mbeleni.
Bongo ukikaza sana fuvu kusema unanunua vitu brand kubwa kwa bei kubwa na umeme wenyewe huu wa tanesco zima washa zima washa utajikuta unapata hasara tu.

Kama TV ina warranty miaka miwili na unainunua 800K kwa sifa zile zile ungezipata kwenye brand kubwa ya 1.2mill mimi bado siioni sababu ya ku-hesitate na hizo siyo kwamba ni mbovu kiasi hiko unaweza ukawa na LG ukaipeleka kwa fundi lakini hiyo MEWE ikabaki inadunda,juzi nimebeba Haier Android wamenipa warranty miaka mitatu nilichofanya nimenunua TV guard isipate shot maana kwenye warranty kesi ya umeme haihusiki.
 
Cheap is costly!

Kwenye vifaa vya electronics, set mbili zinaweza kuwa na sifa sawa, ila tofauti ya workmanship katika matengezo zikawa ni mbingu na ardhi. Kabla hujakaa vizuri solder inapata crack na kukukosesha uhondo wote. Kwa vile wewe siyo fundi, utaishia kupoteza pesa zaidi.
 
TV inch 55 ni kubwa sana kwa matumizi ya nyumbani
Wabongo kinagomba hatuna pa kuziweka hizo tv kwa sababu kwanza tunajenga vijumba vyetu tumevibana bana kiasi nafasi inabaki ndogo mtu anaona bora aweke tv 32" akijifariji bora anaona picha basi inatosha.

Kuna siku nilikuwa na ugeni kwa jamaa yangu aisee ameweka ndani TV 65" hiyo ni habari nyengine acha tu tutafute hela.
 
Chief mkwawa nilimuelewa alishauri sehemu kwamba tv nyingi designed kwa africa ubora wake hawatofautiani , so fanya maamuzi kwa usahihi wa kipato chako
 
Naskia wameshika soko la West Africa ..east Africa ndo wameingia hvi karbun ndomaana wamekuja na strategy ya bei cheap.

ila ukienda Nigeria Ghana Hisense wanaiona kama Mewe halafu Mewe ndo Hisense ya kule

-Maneno ya muuza Tv kariakoo
Fix
 
Hapo kwenye sifa zile zile ndio uongo ulipo mkuu. Ukitaka kuamini, jaribu kudisplay image at the same time.
 
Nimeishi na LG miaka 7 haijawahi haribika kabisaaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…