Hivi ubora wa Yanga unaoimbwa kila wakati uko wapi?

Hivi ubora wa Yanga unaoimbwa kila wakati uko wapi?

Nalazimika kuuliza hili swali kutokana na huu wimbo wa Yanga, kila siku Yanga ni bora, Yanga ni kubwa, wakiingia uwanjani ubora hauonekani.

Walikutana na timu yenye ubora Vipers wakapoteana, wakala 2. Walikutana na timu yenye ubora Simba wakapoteana, japo mpinzani alijivuruga mwenyew kipindi cha pili wakashinda. Ila ilionekana kabisa walipoteana, japo pia huenda kuruka ukuta nako kuliwasaidia.

Walikutana na timu yenye ubora Al Hilal wakalazwa chali. Walikutana na timu yenye ubora kidogo tu ya Azam ikalazimika watoe sare kwa gori la mpira uliotoka nje ila refa akawabeba wakatoa sare.

Kutokana na matokeo haya ya uwanjani, nalazimika tu kuwaza yafuatayo:

1. Je, wanajiona bora kwa sababu wana azizi Ki?
Kama ni hivyo basi wanakosea, maana huyu hana mafanikio yoyote Afrika zaidi ya kushindwa kuipeleka timu yake robo fainali msimu uliopita.

2 . Wanajiona bora sababu wana mayele?
Kama ni hivyo basi wanakosea, maana huyu na wenzake akina Moloko, Juma Shabani na wengine wakiwa na As Vita yao, walikaa nje ndani kwa Simba kwenye CACL na cha ziada ni kwamba, huyo Mayele anayeimbwa hajawahi kupata tuzo yoyote tangu azaliwe.

3. Wanajiona bora kwa sababu wana Morrison?
Kama ni hivyo basi wanakosea, maana huyu pale Simba alilazimika akae benchi mpaka alipoondoka Chama ndipo akapata namba.

4. Je, wanajiona bora sababu wana Fei?
Kama ni hivyo basi wanakosea, maana hana wasifu wowote kimatendo (ya soka) nje na ndani ya nchi labda kwa kuongea tu.

5. Wanajiona bora kwa sababu ya Nabi?
Kama ni hivyo basi wanakosea sana, maana hana rekodi yoyote nzuri tangu aanze kazi ya mpira, sanasana mwaka jana aliitwa Profesa kupitia mgongo wa mtu kisha akakutana na ubingwa wa Yanga wenye mashaka.

Enyi watu wenye ujuzi thabiti wa uchambuzi wa soka, nisaidieni, Yanga wanavyosema wana timu bora kitu gani kitanishawishi nami niamini hivyo?
IMG-20221021-WA0179.jpg
 
Wivu tu umekujaa. Kama timu imemaliza msimu wa ligi, huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote! Ikachukua makombe yote; kuanzia Ngao ya Jamii, Kombe la Ligi Kuu, na Kombe la ASFC!!

Bado utasema hiyo timu haikuwa na kikosi bora. Imewafunga mara 2 ndani ya msimu mmoja!
Mlipofungwa na Al Hilal Sudan na kutolewa ulipotea sana humu 🤣🤣🤣...subiria kesho mkishafungwa kama utarudi humu,na kwa taarifa yako hakuna kocha anayeinyanyasa utoporooo kama Mgunda tangu enzi akiwa Coastal Union
 
Back
Top Bottom