Naomba wana jf mnisaidie.
Nilipokwenda UDOM (University of Dodoma) kwa mara ya kwanza kuona chuo kikubwa ambacho kinavuma kwa kasi. Ukiwa unaingia getini utakutana na nembo kubwa ya CCM wakat vyuo vingne unakutana na nembo ya chuo husika, nikapata maswali bila majibu kua hivi Udom ni chuo cha Umma au CCM?
Hiyo nembo ni ya vyuma na imejengewa zege zito. Nilijaribu kuongea na mmoja wa wanafunzi akanambia wao walishajaribu kulifikisha hilo kwenye utawala tangu 2008, jibu walilopewa ni kua anaeweza akodi buldoza akaitoe ati wao hawawezi kuharibu mamilioni ya pesa.
UDOM ilianzia kwenye jengo la chimwaga ambalo ni la ccm,ndio maana hiyo nembo kuwepo hapo,ila ni vizuri ikaondolewa,by the way,siasa haziruhusiwh vyuoni