Hivi ukicheza soka na timu za majeshi sheria na kanuni za mpira huwa zinaachwa kando?

Sijawahi kusikia mchezaji wa prison kasajiliwa na timu nyingine au kaitwa timu ya taifa, mwenye kumbu kumbu anambie.

Sent from my TECNO BA2 using JamiiForums mobile app
Wewe Utakuwa huwa hufatilii mpira tu!! Chakukusaidia tu mkuu


Salum kimenya keshaitwa karibia mara mbili, Cleofas mkandala kabla hajahama TZPrisons keshaitwa

Hawa ni baadhi ya wachezaji wa Prisons na wakasajiliwa Timu nyibgine


Primus kasonso_Simba
Ismail Aziz_Azam
Kelvin Friday_Biashara
Victor Hangaya_Mbeya city
Cleofas mkandala_Dodoma Jiji
Eliuter Mpepo_alienda singida akaenda Zambia sahv yupo Kati ya msumbiji au Afrika kusini!!
 
Ongezea na Henry Moris na marehemu Godfrey Bonny walienda Yanga
 
Tatizo la kuujulia mpira uzeeni.
Hujui kuwa tumewahi kukufunga tukiwa dhaifu na pungufu uwanjani?

Timu kuwa pungufu kama wana mikakati mizuri wanaweza kushinda mechi kwa magoli ya counter attack.
 
Siku hizi mmekuwa malalamiko FC, chezeni mpira wa kiume siyo kulegea kama mchicha
 
Uto km uto
 
Umeandika point Sana,
Mechi ile Prison walicheza kibabe Sana. Walicheza Kama mechi za kina Ashanti na Boom za ilala enzi hizo. Tukiacha adhabu ya red Card ilipaswa TFF wawapige faini hawa.
 
Vipi refa alivyowapa simba goli ka off side?
Hata offside hiyo sheria yake huifahamu vema simba alinyimwa goli la shuti liliotemwa la Shabalalah na Kopa Mugalu kuzamisha wavuni alikuwa offside.Tuseme tu ukweli sheria ya goli la offside inawachanganya marefa wetu.
 
Mpira wa kihuni unaoutaka mbona tunauweza kuliko nyie.Ni vile wachezaji wetu wanajitambua kwani hapo sio mahali pa kuonesha miguvu na uhuni.Soka ni sehemu ya kuonesha skills na ubunifu unaoleta burudani,sio kuingia kama kondoo kisa una fuvu gumu
Siku hizi mmekuwa malalamiko FC, chezeni mpira wa kiume siyo kulegea kama mchicha
 
Mbona simba iliwahi wafunga Yanga ikiwa Pungufu? Umesahau Yanga mwenzangu?ninyi mmechelewa sana kuufahamu mpira ila ni mashabiki wa simba na yanga tu. Mimi ninapenda mchezo wa mpira wa miguu na kuipenda yanga. Ndo maana hunikuti nikishabikia upuuzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…