Hivi ukigundua umeibiwa funguo ya gari unafanyeje?

Mlolongo

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2019
Posts
3,483
Reaction score
6,257
Juzi usiku mnene kuna kibaka/vibaka waliruka ukuta wakaingia maskani.

Fast forward: Alfajiri niliamka nikakuta madirisha (vioo) vimefunguliwa. Sebuleni wakaiba box la simu (wakidhani kuna simu ndani), chumbani wakachomoa kadeti zangu nne, mashati mawili yalikuwa karibu na dirisha.

Lakin pia nikagundua ufunguo wa babywoka yangu umeanguka kutoka kwenye dressing table. Ni kama walijaribu kuuvuta kwa kutumia fimbo ukaanguka wakaachana nao.

Nikawaza wangefanikiwa kusepa na funguo ingekuwaje, wangewasha gari ambalo lipo uani? Geti wangefunguaje? Wasingeweza kuondoka nalo, nyumba nzima tungesikia bila shaka.

Off course ninayo spare key. Lakin vipi hii funguo original ambayo wangesepa nayo... Usalama wa gari yangu si ungekua kwenye mhaho!!

Hivi wakuu, ikitokea umegundua umeibiwa funguo yako ya gari unatakiwa ufanyeje immediately? Unamuita fundi anabadili Starter? Gharama zake kwa vigari vidogo inaweza kucheza kwenye shingapi, laki moja inazidi?
 
Picha ya gari
 
Unakwenda kwa mafundi funguo unabadilisha meno ya ugunguo so ugunguo wa zamani unakua hauwezi kufanya kazi tena
 
Swali zuri sana.

Nilishawahi waza kitu kama hiki. Na mbaya zaidi uende sehemu upaki gari na upoteze funguo. Unaweza zimia.

Nikazidisha umakini na funguo wa gari.
 
Kuna maduka mitaa ya uhindini wanauza full pack. Yaani unabadilishiwa starter, lock za milango yote panapohitaji funguo.

Sijajua gharama yake na uimara wa maeneo hayo baada ya kubadilishwa.

Binafsi sijawahi badili mfumo wa funguo wa gari.

Ila nimecheka sana, asante kwa jioni tulivu.
 
Na kwanini ulale kizembe mwanaume unaibiwa hata hisia huna
Radio ndio chanzo. Niliacha radio inapiga muziki kwa mbali + sauti ya feni halafu na mvua palikuwa na manyunyu.
 
watu walivyo ona upo kimya wakasema wewe ndie mama Samia
 

Starter has nothing to do with wewe kuibiwa gari.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…