Hivi ukikopa benki (as mtumishi wa serikal) halafu ukaacha kazi, je unaweza ukafuatiliwa?

Hivi ukikopa benki (as mtumishi wa serikal) halafu ukaacha kazi, je unaweza ukafuatiliwa?

Mkuu kuna vigezo vya kupewa ndio maana wanaomba barua ya kuthibitishwa kazini ,miaka uliyofanya kazi na kiwango chako cha mshahara kwa mwezi kifupi huwezi pata mkopo unaozidi mafao yako
Kinachofanya ukopwe fedha nyingi au chache (kulingana na mtu unavyoona kuwa ni nyingi au chache) ni kiwango cha mshahara unaochukua kwenda nacho nyumbani (net salary) na sio kiwango cha mafao yako, mikopo ya watumishi dhamana ni mshahara, pensheni ni moja ya sehemu tu lakini mfuko wa jamii kama haukushirikishwa katika mapatano ya huo mkopo wenu unaweza kukataa kumpa mdai sehemu ya fedha za mtumishi kwa kuwa mahusiano ni kati ya mfuko na mtumishi na sio watu wengine, labda kama watakuja na amri ya mahakama
 
Hili ndio swali la msingi,maana pale kwenye mkopo kuna charges za insurance against hip mkopo
Watu wachache wanaoibua hoja ya bima mahakamani, kwa kesi kama tatu nilizoshuhudia wamekuwa wakifanikiwa, unachotakiwa kufanya ni kuomba kampuni ya bima iwe sehemu ya kesi husika..hapo mabenki huwa hawarudi tena mahakamani
 
Bima ya mkopo hucover kifo tu. Na pia mafao hayatumiki kulipa mkopo wowote wa bank isipokua ile mikopo ambayo mfuko kwa kushirikiana na bank hutoa kama product kwa wanachama wake.
 
Swali,,umekopa ukaacha kazi,,after 7 years ukarudi kazini Mkopo utaendelea kukatwa??
 
Back
Top Bottom