Hivi ukikopa trekta unaweza toboa?

Hivi ukikopa trekta unaweza toboa?

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
Wazo la kukopa trekta HP 50 kulima mashamba yako kukodisha Mara chache ili upate mafuta.Kulima heka 600 yaani eka 20 kwa siku.

Mazao ni yale yasiyo na changamoto nyingi mfano kunde, karanga,mtama,mihogo,viazi vitamu,mbaazi,njugu. mategemeo ni gunia 1000 kwa msimu mmoja wa zao moja wapo.

HP 50 new tractor brand New Holland, Case, John Deere si zaidi ya milion 60.

Mkopo ndani ya mwaka mmoja. Je, itawezekana kurejesha mkopo? Maana hesabu za makaratasi ukiingia field ni tofaut.

Dereva ni wewe mwenyewe unakomaa nalo heka 20 kwa siku unapumzika.

Kulima ni saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi na saa kumi jioni hadi saa nne usiku kupumzika ni masaa nane tu

Vipi walio na uzoefu, je utatoboa?

Kwann mazao hayo ni kwa sababu Sio complicated yaani hata kwa mvua chache unavuna hayachagui udongo, hayahitaji mbolea Wala madawa. Pia Sio mazao pendwa kulogwa na wachawi vijijini labda Yana ukinzani.

Nipeni idea.
 
Wazo la kukopa trekta HP 50 kulima mashamba yako kukodisha Mara chache ili upate mafuta.Kulima heka 600 yaani eka 20 kwa siku.
Mazao ni yale yasiyo na changamoto nyingi mfano kunde, karanga,mtama,mihogo,viazi vitamu,mbaazi,njugu. mategemeo ni gunia 1000 kwa msimu mmoja wa zao moja wapo.
HP 50 new tractor brand New Holland,Case, John Deere si zaidi ya milion 60.
Mkopo ndani ya mwaka mmoja.
Je itawezekana kurejesha mkopo?
Maana hesabu za makaratasi ukiingia field ni tofaut.
Dereva ni wewe mwenyewe unakomaa nalo heka 20 kwa siku unapumzika.
Kulima ni saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi na saa kumi jioni hadi saa nne usiku kupumzika ni masaa nane tu
Vipi walio na uzoefu je utatoboa?
Kwann mazao hayo ni kwa sababu Sio complicated yaani hata kwa mvua chache unavuna hayachagui udongo,hayahitaji mbolea Wala madawa,Pia Sio mazao pendwa kulogwa na wachawi vijijini labda Yana ukinzani.
Nipeni idea.

Weka hata space kidogo kwenye maandishi yako
 
Kama unalimia watu mashamba unaweza kutoboa japo inategemea na msimu wenyew na watu wa huko
 
Wachawi, saa kumi usiku, mwaka mmoja,

Tafta mwenye anajua kupangilia mawazo afu wew ufanye kubinya tu hapo kwenye button ya send
 
Ni ngumu sana kumaliza uo mkopo kwa mwaka mmoja walau upewe ata miaka mitano coz Kuna ups and downs

Inawezekana lakini inahitaji uzoefu sana kwenye gemu pia hakuna zao linalovumilia ukame ila kunazao linalohitaji mvua chache

Heka 20 kuanzia saa kumi hadi saa tano haiwezekani

Kufupisha mada tafuta wazoefu hizo kazi wakupe hint you seem to be too shallow kwenye kilimo
 
Ml 60 kwa mwaka uwe umerejesha zote!?
Au unapanda mkonge?
napo bado acha utani wewe siku hizi mazao yote ya chakula na mboga mboga yanahitaji madawa.
 
Na mifano ya watu wawili wa karibu. Mmoja alikopa kama wewe akalipeleka morogoro akamwachia ndugu yake wa damu akawa anapiga mzigo kuwalimia watu mashambaYao.
Baada ya muda trekta likawa halifai kifupi haikumlipa deni anadaiwa. Lakini anadai alihujumiwa na huyu ndugu yake.
Mfano wa pili huyu ni mstaafu ambaye aliamini kwenye kilimo. Alipopata mafao akanunua na kulipeleka mahenge.
Mpaka sasa bado ramani hazichori japo msimamizi ni mwenyewe na amehamisha makazi kabisaa.
Kifupi sikushauri uingie kwenye shughuli yoyote ya kilimo kwa pesa ya mkopo.
 
Plan za makaratasi versus uhalisia kwenye field. Kikubwa ni nia tu sema kilimo sio kulima tu kuna masoko ndio kuna impact ya kile unachofanya
Soko Sio ishu lipo tele ndani na nje
 
Ml 60 kwa mwaka uwe umerejesha zote!?
Au unapanda mkonge?
napo bado acha utani wewe siku hizi mazao yote ya chakula na mboga mboga yanahitaji madawa.
Karanga,kunde viazi vitamu je
 
Kwa Aina ya mazao uliyotaja hapo huwez kutoboa labda uwe unauhakika wa soko...
Unajua hyo mil 60,wanakupa trekta na halo basi......
Rotta hawakupi wala jembe hupewi..
Labda Kama utatoa kianzio zaidi ya 45mil hapo utalikomboa
 
Wazo la kukopa trekta HP 50 kulima mashamba yako kukodisha Mara chache ili upate mafuta.Kulima heka 600 yaani eka 20 kwa siku.
Mazao ni yale yasiyo na changamoto nyingi mfano kunde, karanga,mtama,mihogo,viazi vitamu,mbaazi,njugu. mategemeo ni gunia 1000 kwa msimu mmoja wa zao moja wapo.
HP 50 new tractor brand New Holland,Case, John Deere si zaidi ya milion 60.
Mkopo ndani ya mwaka mmoja.
Je itawezekana kurejesha mkopo?
Maana hesabu za makaratasi ukiingia field ni tofaut.
Dereva ni wewe mwenyewe unakomaa nalo heka 20 kwa siku unapumzika.
Kulima ni saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi na saa kumi jioni hadi saa nne usiku kupumzika ni masaa nane tu
Vipi walio na uzoefu je utatoboa?
Kwann mazao hayo ni kwa sababu Sio complicated yaani hata kwa mvua chache unavuna hayachagui udongo,hayahitaji mbolea Wala madawa,Pia Sio mazao pendwa kulogwa na wachawi vijijini labda Yana ukinzani.
Nipeni idea.
Usijaribu hailipi kazi ya matrekta ni hovyo kabisa fanya biashara ya uhakika.
 
Unaweza utoboe au ukatoboka, inategemea

Kama kilimo chako kinategemea mvua iyo ni kamali, ila kama unategemea umwagiliaji na mvua unaweza kutoboa,
Kulima kwa kutegemea mvua kwa miaka ya Sasa ni hasara sana kwani mvua zime kuwa sizo zenye kueleweka

Kama una mwagilii uhakika ni mkubwa Sana
 
Back
Top Bottom