Hivi ukikopa trekta unaweza toboa?

Hivi ukikopa trekta unaweza toboa?

M nimewah simamia trekta magu uko tulikua tunalima kwa msimu kule hakuna kupoa wanalima kila siku yaan wakimaliza wanahamia sehem zingn kama morogoro,nyamongo,shinyanga yaan wanahama na msimu kuna jamaa wanazo mpk trekta 7 anapiga pesa tu ukiwekea na tela lake unabeba mazao shamban ata magogo au pumba sio mbaya.
 
Ukikubali kujitoa itakutoa, ila siyo umalize mkopo kwa mwaka mmoja. Kama ni miaka 3 sawa, maana trekta iko na kazi Jan mpaka Dec inapiga kazi tu.

Mwezi wa tisa inaanza kilimo mpaka April kwenye Dengu, baada ya hapo inashusha Jembe na kufunga Tera, inaanza kubeba mizigo ya magunia ya Nafaka toka porini kuleta Senta au Mjini.

Mwezi wa saba inaanza kusomba Dengu na kupiga, mwezi wa nane kati kati unapiga service then mwezi wa tisa inabeba tena Jembe.

Ni hayo tu maseee.
 
Kama hilo shamba ulilosema 600 acres lina chanzo cha uhakika cha maji

tractor liwe na jembe , harrow na tellar

Basi iyo pesa inarudi chap mwaka mmoja tu hukosi 300 m

Nitafute tufanye kazi
 
Kwanini mnakimbilia mikopo? Kwa sababu mnaona ni njia rahisi ya kutoboa kumbe mnajidanganya
Ni sawa na kusema huwezi kuwa tajiri mpaka uwe mwizi au ushirikina

Vijana hela zinatafutwa msiwe na tamaa za haraka haraka

Weka malengo yako hata kwa biashara ndogo utakayoikuza kwa miaka kadhaa huku ukiwa na lengo la kuweka akiba kwa ajili ya mpango wako mwingine kwa mfano hilo [emoji609]

Ukikopa eti ulipe kwa mwaka huku ukiwa huna mradi wowote unajidanganya
 
Wazo la kukopa trekta HP 50 kulima mashamba yako kukodisha Mara chache ili upate mafuta.Kulima heka 600 yaani eka 20 kwa siku.

Mazao ni yale yasiyo na changamoto nyingi mfano kunde, karanga,mtama,mihogo,viazi vitamu,mbaazi,njugu. mategemeo ni gunia 1000 kwa msimu mmoja wa zao moja wapo.

HP 50 new tractor brand New Holland, Case, John Deere si zaidi ya milion 60.

Mkopo ndani ya mwaka mmoja. Je, itawezekana kurejesha mkopo? Maana hesabu za makaratasi ukiingia field ni tofaut.

Dereva ni wewe mwenyewe unakomaa nalo heka 20 kwa siku unapumzika.

Kulima ni saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi na saa kumi jioni hadi saa nne usiku kupumzika ni masaa nane tu

Vipi walio na uzoefu, je utatoboa?

Kwann mazao hayo ni kwa sababu Sio complicated yaani hata kwa mvua chache unavuna hayachagui udongo, hayahitaji mbolea Wala madawa. Pia Sio mazao pendwa kulogwa na wachawi vijijini labda Yana ukinzani.

Nipeni idea.
Labda ungesema pia hayo mashamba yako wapi? Kusema ukweli inategemea na sehemu unakolimia! Kwa mfano Manyara, Katavi, Sumbawanga, Songwe n.k ambako mvua ni za uhakika. Nina ushahidi wa watu waliojitoa kwenye Kilimo wakatoboa! Kama una uhakika wa kuwa na mashamba makubwa ya kwako yawe hata ya kukodi huko Manyara nenda kalime mahindi, ngano, safflower (Carthamus). Bila shaka kabisa unatoboa. Sehemu nzuri kwa Kilimo cha mahindi na ngano ni Hanang' sehemu inaitwa Dirmar kukodi shamba zuri kabisa ni 150k per acre (haya ni maeneo ya uhakika kuvuna). Kodisha kama ekari 100 hivi piga mahindi yako au ngano halafu utaleta mrejesho hapa kama hautakuwapo mchoyo.
 
Ukikubali kujitoa itakutoa, ila siyo umalize mkopo kwa mwaka mmoja. Kama ni miaka 3 sawa, maana trekta iko na kazi Jan mpaka Dec inapiga kazi tu.

Mwezi wa tisa inaanza kilimo mpaka April kwenye Dengu, baada ya hapo inashusha Jembe na kufunga Tera, inaanza kubeba mizigo ya magunia ya Nafaka toka porini kuleta Senta au Mjini.

Mwezi wa saba inaanza kusomba Dengu na kupiga, mwezi wa nane kati kati unapiga service then mwezi wa tisa inabeba tena Jembe.

Ni hayo tu maseee.
Ni mkoa gani huu mkuuu ???
 
Back
Top Bottom