Mimi na jirani zangu mbona hatuna?
Labda ungesema pia hayo mashamba yako wapi? Kusema ukweli inategemea na sehemu unakolimia! Kwa mfano Manyara, Katavi, Sumbawanga, Songwe n.k ambako mvua ni za uhakika. Nina ushahidi wa watu waliojitoa kwenye Kilimo wakatoboa! Kama una uhakika wa kuwa na mashamba makubwa ya kwako yawe hata ya kukodi huko Manyara nenda kalime mahindi, ngano, safflower (Carthamus). Bila shaka kabisa unatoboa. Sehemu nzuri kwa Kilimo cha mahindi na ngano ni Hanang' sehemu inaitwa Dirmar kukodi shamba zuri kabisa ni 150k per acre (haya ni maeneo ya uhakika kuvuna). Kodisha kama ekari 100 hivi piga mahindi yako au ngano halafu utaleta mrejesho hapa kama hautakuwapo mchoyo.Wazo la kukopa trekta HP 50 kulima mashamba yako kukodisha Mara chache ili upate mafuta.Kulima heka 600 yaani eka 20 kwa siku.
Mazao ni yale yasiyo na changamoto nyingi mfano kunde, karanga,mtama,mihogo,viazi vitamu,mbaazi,njugu. mategemeo ni gunia 1000 kwa msimu mmoja wa zao moja wapo.
HP 50 new tractor brand New Holland, Case, John Deere si zaidi ya milion 60.
Mkopo ndani ya mwaka mmoja. Je, itawezekana kurejesha mkopo? Maana hesabu za makaratasi ukiingia field ni tofaut.
Dereva ni wewe mwenyewe unakomaa nalo heka 20 kwa siku unapumzika.
Kulima ni saa kumi usiku hadi saa tano asubuhi na saa kumi jioni hadi saa nne usiku kupumzika ni masaa nane tu
Vipi walio na uzoefu, je utatoboa?
Kwann mazao hayo ni kwa sababu Sio complicated yaani hata kwa mvua chache unavuna hayachagui udongo, hayahitaji mbolea Wala madawa. Pia Sio mazao pendwa kulogwa na wachawi vijijini labda Yana ukinzani.
Nipeni idea.
Ni mkoa gani huu mkuuu ???Ukikubali kujitoa itakutoa, ila siyo umalize mkopo kwa mwaka mmoja. Kama ni miaka 3 sawa, maana trekta iko na kazi Jan mpaka Dec inapiga kazi tu.
Mwezi wa tisa inaanza kilimo mpaka April kwenye Dengu, baada ya hapo inashusha Jembe na kufunga Tera, inaanza kubeba mizigo ya magunia ya Nafaka toka porini kuleta Senta au Mjini.
Mwezi wa saba inaanza kusomba Dengu na kupiga, mwezi wa nane kati kati unapiga service then mwezi wa tisa inabeba tena Jembe.
Ni hayo tu maseee.