Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,367
- 11,604
Ee, nimempatia simu aandike namba yake, akaishia kushtuka shtuka tu, mara ang'ate vidole, mara aangalie chini kushoto. Nikamwambia acha kanjanja, chora namba kwa simu hapo. Mara ooh, mi siwezi, mara ooh huna nia nzuri na mimi, mara oh ya kazi gani
Nikamwambia kama hutaki nipatie simu yangu, akaanza mi nakupa lakini sijawahi, mara ooh usinipigie simu usiku, kwetu tumelelewa kwenye misingi ya dini, mara au basi, utanipigia tu. Mtoto kachora namba
Dakika 5 ni nyingi kaanza kujipitisha, mara aende mata arudi, akienda ana gauni la kijivu, akirudi ana kijinzi cha mwendokasi, akienda kashikilia dera, akirudi kashikilia kipochi manyoya. Kha! Ikabidi nimuite nimgee fruti achambe koo
Kama mjuavyo kwenye mafanikio hapakosekani wanga, mdudu kidukulio a.k.a mende akaonekana kwenye fruti akisherehekea mwanzo wa penzi jipya. Hakukua na namna zaidi ya kumpotezea
Ni hayo tu. Karibuni hapa Riverside tuendelee kupata mvinyo...