Hivi ukubwa Simba SC uko wapi?

Kamgomoli

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2018
Posts
1,896
Reaction score
4,058
Haji Manara anajitapa,mashabiki wanajitapa,viongozi wanajitapa kwamba Simba ni klabu kubwa. Hv ukubwa Simba uko wapi labda wenzangu mnisaidie.Yaani kufika robo fainali Caf champions ligi baada ya miaka zaidi ya 15 ndo mnajimwambafai kwa kiasi hicho? Vipi TPMazembe au Vita wasemeje? Kujiona wakubwa ndio maana mnafukuza makocha ovyo ovyo huku mnaongoza ligi, maajabu ya Dunia aisee. Hv mnaelewa maana ya ukubwa wa club?

Club inaendeshwa kwa majungu na fitina na bila weledi ukubwa wake uko wapi? Ni kweli Simba km ilivyo kwa Yanga ni miongoni mwa timu maarufu Africa mashariki na Afrika kwa ujumla lakn si kubwa kiivo. Kuna mengiiii sn ya kuendelea kujifunza ili kuufikia huo ukubwa wanaoutaja.

Shida tunajidanganya sn, Ausems kaondoka kwa sababu ya uchanga wa club zetu ambazo hazitaki kujifunza miaka nenda rudi. Kwa staili hii mspobadilika Simba itarudi tena robo fainali baada ya miaka 15.
 
Umejitahidi Leo, umeongea pumba yenye chengachenga zinazofaa kwa kuku wanao taga,πŸ˜†πŸ˜† hebu chukua sumu ya panya hapo dukani nakuja kulipia kesho wakati wa kuzika...
 
Bila shaka unawashwa.
 
Afrika tuna timu zaidi ya 200, kwenye rank Simba/Lunyasi/Mnyama iko namba 16
Unashindwa kuiita timu kubwa kwasababu zipi tena bwashee?
 
Afrika tuna timu zaidi ya 200, kwenye rank Simba/Lunyasi/Mnyama iko namba 16
Unashindwa kuiita timu kubwa kwasababu zipi tena bwashee?
Hivyo kuwa namba 16 ndio ukubwa Mkuu? πŸ€”πŸ€”πŸ€”
 
Nakuunga mkono,Simba imefanya upuuzi wa hali ya juu.
 
Povu la nini? Kama ndogo basi nyamaza. Nenda uarabuni, brazil, marekani raia wa huko timu ya tanzania kisa subiri jibu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…