Hivi Ulaya kuna utaratibu wa kuulizwa jina la balozi wa mtaa/mtendaji kata, diwani au mbunge ili kuthibitisha kama ni mkazi wa sehemu husika?

Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.

Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.

Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? Kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.

Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?

Muhimu utakuepusha na mambo na adha Kama hizo,
 
Ok.Haujapenda kutanua mjadala tu.Ngazi ya kitongoji,Kijiji,mtaa hakuna wadhifa wa balozi.Mabalozi wamebaki wa CCM tu ili kuwahamasishia mambo yao kichama.
chaguzi za serikali za mitaa huchagua watu nafasi gani?

kwa vijijini tuna nafasi 3 (mwenyekiti wa kijiji, tuna kitongoji na tuna balozi),

kwa mijini tuna mwenyekiti wa mtaa, tuna balozi.... (hio ya kitongoji mjini sijaisikia),

balozi ni mtu muhimu sana kwenye structure ya uongozi hapa nchini, yeye ndiye mwenye watu!
 
Nikiwa narudi zangu ghetto imebidi nipite shortcut bahati mbaya nimekosea njia nakujikuta napita njia ya kwenda uhani kwa mtu sio mzuri kwenye vichochoro vya mjini sasa wahusika wakaanza kuwa na mashaka na mimi.

Wakaniweka mtu kati nakuanza kuniuliza maswali with confidence nikawaelezea kuwa naelekea nyumbani ila bahati mbaya nimekosea njia.

Wakaanza kuniuliza balozi wako anaitwa nani? Kimsingi sio kwa ubaya licha ya kuishi huu mtaa simjui balozi, mtendaji wala diwani. wakanituhumu kuwa mimi nitakuwa mtu mbaya na sio mkazi wa sehemu husika kisa simjui balozi.

Hivi kweli kwa ingia na kutoka ya jiji hili la Dar es salaam jumlisha wingi wa watu pamoja na harakati za kimaisha kuna umuhimu gani wa kuulizana majina ya viongozi wa ngazi za chini?
Usemi wako unaonesha ulikuwa unawinda mke wa mtu.
 
Back
Top Bottom