Uchaguzi 2020 Hivi umati wote wanaomshabikia Lissu ni wapiga kura? Je, wanavyo vitambulisho vya kura?

Uchaguzi 2020 Hivi umati wote wanaomshabikia Lissu ni wapiga kura? Je, wanavyo vitambulisho vya kura?

Narumu kwetu

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Posts
1,888
Reaction score
4,489
Ukiona umati mkubwa wa vijana wanataka mabadikiko kweki kweli, hali ni ngumu mtaani, ajira ni ngumu sana, biashara ni ngumu, kazini mishahara haikidhi mahitaji ya soko, wanaonufaika na uchumi wa kati ni wachache, hosptalini hata panadol ni adimu.

Lakini kama hatujui tunalofanya tutaweza kuyapata mabadikiko? Hivi umati wote wanaomshabikia Lissu ni wapiga kura? Je, wanavyo vitambulisho vya kura? Je, upinzani unafahamu umuhimu wa tume huru? Je upinzani wanafahamu uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura haliko updated?

Si kwa sasa labda 2030 kidogo upinzani unaweza ukawa na nguvu. Ieleweke nguvu si watu pia katiba mpya na maboresho ya daftari la kura ni nguvu kubwa pia.
 
CCM mna propaganda za kijinga sana. Sasa wewe unajuaje kama umati uliopo kwa Lissu hawajajiandikisha?

Yani unasema kwa uhakika kabisa Eti hao hawana vitambulisho vya kupiga kura. Hizo propaganda zenu nawaambia mwaka huu zimefeli big time.

Na CCM ijiandae tu kukabidhi nchi kwa Tundu Antipas Lissu!
 
CCM mna propaganda za kijinga sana. Sasa wewe unajuaje kama umati uliopo kwa Lissu hawajajiandikisha? Yani unasema kwa uhakika kabisa Eti hao hawana vitambulisho vya kupiga kura. Hizo propaganda zenu nawaambia mwaka huu zimefeli big time.

Na CCM ijiandae tu kukabidhi nchi kwa Tundu Antipas Lissu!
Mkuu kumeshakucha naona uko ndotoni
 
CCM mna propaganda za kijinga sana. Sasa wewe unajuaje kama umati uliopo kwa Lissu hawajajiandikisha? Yani unasema kwa uhakika kabisa Eti hao hawana vitambulisho vya kupiga kura. Hizo propaganda zenu nawaambia mwaka huu zimefeli big time..
Umati ukiwa mkubwa upande wa CCM inaonekana wamejiandikisha. shame on them
 
Umati ukiwa mkubwa upande wa CCM inaonekana wamejiandikisha. shame on them
Wajinga sana hawa jamaa! Na mbaya zaidi wanataka kutufanya watanzania wote kuwa wajinga kuamini propaganda zao uchwara!!
 
Ukiona umati mkubwa wa vijana wanataka mabadikiko kwekikweli, hali ni ngumu mtaani, ajira ni ngumu sana, biashara ni ngumu, kazini mishahara haikidhi mahitaji ya soko, wanaonufaika na uchumi wa kati ni wachache, hosptalini hata panadol ni adimu...
Hao vijana baba zao,mama zao,majirani zao,watumishi wa umma na wafanyabiashara ni wateja wao
 
Ukiona umati mkubwa wa vijana wanataka mabadikiko kwekikweli, hali ni ngumu mtaani, ajira ni ngumu sana, biashara ni ngumu, kazini mishahara haikidhi mahitaji ya soko, wanaonufaika na uchumi wa kati ni wachache, hosptalini hata panadol ni adimu...

Kwa taarifa yao tume, wapiga kura watanzania ni 29m+, yaani nusu ya watanzania wote wanaokaribia 60m. Hapa ninapata shaka sana kuwa watu wenye umri wa miaka 18+ ni sawa kabisa na walio chini ya 18yrs! Halafu cha ajabu nusu ya watanzania wote wawe wamejiandikisha kupiga kura! Yajayo yanafurahisha.
 
wengi wao hawana vitambulisho vya kupigia kura ,,,, wakati wa kuupdate daftari la kudumu mapema January mwaka huu wapinzani wengi walisusia makusudi sijui walikuwa na malengo ya kumkomoa nani
 
Ukiona umati mkubwa wa vijana wanataka mabadikiko kwekikweli, hali ni ngumu mtaani, ajira ni ngumu sana, biashara ni ngumu, kazini mishahara haikidhi mahitaji ya soko, wanaonufaika na uchumi wa kati ni wachache, hosptalini hata panadol ni adimu.

Lakini kama hatujui tunalofanya tutaweza kuyapata mabadikiko? Hivi umati wote wanaomshabikia Lissu ni wapiga kura?, Je wanavyo vitambulisho vya kura? Je upinzani unafahamu umuhimu wa tume huru? Je upinzani wanafahamu uandikishaji wa daftari la kudumu la mpiga kura haliko updated?

Si kwa sasa labda 2030 kidogo upinzani unaweza ukawa na nguvu. Ieleweke nguvu si watu pia katiba mpya na maboresho ya daftari la kura ni nguvu kubwa pia.
nimekupa "thanks" kwa ajili ya kichwa cha uzi wako tu na si content ya uzi.

umeuliza swali zuri na muhimu sana.

Cc
CHADEMA
John Mnyika
 
wengi wao hawana vitambulisho vya kupigia kura ,,,, wakati wa kuupdate daftari la kudumu mapema January mwaka huu wapinzani wengi walisusia makusudi sijui walikuwa na malengo ya kumkomoa nani

Kwa mujibu wa idadi ya wapiga kura 2010 walikuwa 15m+, 2015 walikuwa 22m+, na mwaka huu ni 29m+. Pitia vizuri kila uchaguzi kuna ongezeko la wastani wa watu 7m kutoka uchaguzi mmoja mpaka mwingine. Sasa kwa hayo maelezo yako ni aidha tume imepika idadi ya wapiga kura, au idadi kubwa ya watu hawapigi kura.

Fuatilia vizuri, idadi ya wapiga kura wa 2010 na 2015. 2015 walijiandikisha kupiga ni 15m+ walipiga kura ni 11m+. 2015 waliojiandikisha ni 22m+, waliopiga kura ni 15m+. Hiyo maana yake ni watu 7m hawakupiga kura, kwa maneno marahisi 1/3 hawakupiga kura. Kwa mtiririko huo wa watu kutokupiga kura, ina maana wapiga kura wa mwaka huu hawatazidi 24m, na hii ni iwapo Lisu hataenguliwa kugombea uchaguzi. Iwapo Lisu ataenguliwa kugombea uchaguzi huu, wapiga kura watakuwa chini ya 10m.

Sasa ninataka utuambie, kama wapiga kura wa sasa ni 29m+, huku wapinzani hawakujiandikisha, je wangejiandikisha idadi ingekuwa wapiga kura wangapi? Zingatia ukweli ya kuwa watanzania tunakaribia 60m, huku 29m+ wamejiandikisha, yaani nusu ya watanzania wote. Je ni kweli nusu ya watanzania wote wana miaka 18 na kuendelea? Na wote wanaweza kujiandikisha kupiga kura? Kama unatafakari vizuri unaweza kujua uchaguzi huu ni kiini macho.
 
Back
Top Bottom