๐—›๐—ถ๐˜ƒ๐—ถ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ ๐—ง๐˜ƒ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐—จ๐—ป๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ผ๐˜๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ๐—บ๐—ฎ?๐Ÿ˜ณ๐Ÿ”

๐—›๐—ถ๐˜ƒ๐—ถ ๐˜‚๐—ป๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ ๐—ง๐˜ƒ ๐—ฌ๐—ฎ๐—ธ๐—ผ ๐—ถ๐—ป๐—ฎ๐—ท๐˜‚๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐—น๐—ฎ ๐—ธ๐—ถ๐˜๐˜‚ ๐—จ๐—ป๐—ฎ๐—ฐ๐—ต๐—ผ๐˜๐—ฎ๐˜‡๐—ฎ๐—บ๐—ฎ?๐Ÿ˜ณ๐Ÿ”

Teknolojia ni Yetu sote

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2020
Posts
1,386
Reaction score
2,833
ce69517eda4d4f255563f6bdabdbfe04.jpg


Watu wengi wanadhani Smart TV ni kifaa cha kuangalia filamu na vipindi tu, lakini kuna jambo ambalo huenda hulijui! ๐Ÿ‘€

Baadhi ya Smart TV zina teknolojia inayoitwa Automatic Content Recognition (ACR), inayoweza kutambua maudhui unayotazama na kukusanya taarifa hizo kwa ajili ya matangazo, uchambuzi na mapendekezo ya maudhui.

2_20261029_180718_0001.png
3_20261029_180718_0002.png
4_20261029_180718_0003.png


๐Ÿ˜ฑ Jambo la kushangaza ni kwamba, baadhi ya TV zinaweza kutambua hata maudhui yanayotoka kwenye vifaa vya nje kama PlayStation kupitia waya uliyochomeka kama vile HDMI! Nk.

๐Ÿ” Habari njema ni kwamba, baadhi ya TV zinakupa chaguo la kuzima ufuatiliaji huu kupitia mipangilio ya faragha. Hata hivyo, si kila TV hufanya kazi kwa njia sawa.

5_20261029_180718_0004.png
6_20261029_180718_0005.png


Ingia setting kwenye Tv Yako >> Tafuta sehemu ya Privacy, Terms & Privacy au Privacy Choices.

7_20261029_180718_0006.png


Sogeza picha kuona zaidi โœ๏ธ usisahau kutu follow si unajua Teknolojia ni Yetu sote ๐Ÿซก.
 
Du....!! Simekuwa kama smartphone
Sasa ukiwa na simu ya Android na ukawa na Google TV au Android TV si upo kwenye cycle ile ile tu ya kufatiliwa ni kama ume rahisisha zaidi kazi iwe nyepesi ๐Ÿ˜๐Ÿ˜ kwa kuwa na vifaa viwili bab kubwa na bwana mdogo.... N'way tuishi tu wazee kama data zetu wanazo nyingi mno...
 
Kama simu tu. Nadhani haishangazi sana kwa sababu tayari tv ishakua smart hakuna njia inaweza kuwa tofauti sana na smartphone kitabia.
 
Back
Top Bottom