Kuna watu hawa wakukosee vipi lazima uwasamehe.
Msamaha ni Moja ya Njia kuu za kufuta Laana.
Mzazi
Mtoto
Ndugu
Mke(kama hajafanya kosa la ku-cheat)
Hao lazima usamehe ili kuondoa Laana kwenye Familia.
1. Kisa cha Rejea
Yusufu alipotaka kuuawa, kisha kuuzwa na ndugu zake.
Mwisho wa siku alifanikiwa, akasamehe ndugu zake ingawaje hakuwaweka karibu Sana, aliwatafutia eneo zuri la malisho, huko Gosheni. Ili wakafuge mifugo na kulima huko. Huku yeye akibaki IKULU.
Ile ndio ilikuwa Nafasi nzuri ya yeye kulipa Kisasi lakini hakufanya hivyo.
Laana ya kuuzana ndani ya Israel ilikomeshwa na Yusufu.
Kama Yusufu angebaki na Kinyongo Mpake Leo Wayahudi wangekuwa wanasalitiana wao kwa Watu wengine(mataifa mengine)
Lakini Hilo kwa sasa hakipo.
Wayahudi wanasalitiana wao kwa wao au kugombana wao kwa wao lakini kuuzana au kujiunga na mmataifa ili amuuze mwenzake Hilo utasubiri Sana.
Rejea Kwa Musa alipozaliwa na kukulia jumbo la kifalme la Wamisri lakini hakuwasaliti ndugu zake.
Rejea Kisa cha Malkia Esther
Lakini Mtu ametelekezwa na Baba yake au Mama yake hakuwa Responsible Sana kwake. Mtoto akishafanikiwa badala amsamehe mzazi wake hata asipomuweka karibu lakini kumsaidia na kumpa Ile hadhi yake hataki, anataka kumkomesha.
Hiyo Laana inatembea kizazi hata kizazi.
Watu wasameheane