Hivi usipokwenda jkt itakuwaje?

Hivi usipokwenda jkt itakuwaje?

Lengo la vijana kujiunga JKT lilikuwa zuri na still ni zuri seam usimamiaji wa zoezi husika ndio umekuwa mbovu kiasi cha kukuvunjeni moyo ambao bado hamjajienroll na mafunzo!

Moja ya vyombo vilivyoundwa na Serikali ya Tanganyika mara tu baada ya Taifa hili kupata uhuru ni Jeshi la Kujenga Taifa lililoasisiwa tarehe 10 Jul 1963. Jeshi la Kujenga Taifa kwa kifupi JKT, liliundwa ili kuponya majeraha yaliyoachwa na serikali ya kikoloni miongoni mwa jamii ya watanzania ambayo ni pamoja na
ubaguzi wa kidini, makabila, rangi na kipato. Chombo hiki ni muhimu katika kuelimisha na kuandaa vijana wa kitanzania kiuzalendo, kimaadili, kinidhamu na kuwafanya wawe raia wema wanaopenda kutumikia na kulinda nchi yao!

Kupitia JKT, vijana watalelewa vizuri katika malezi yaliyo bora wakiwa wenye:-

(1). Nidhamu
(2). Kujiamini
(3). Moyo wa uzalendo na kuipenda nchi yao
(4). Umoja na Udugu
(5). Moyo wa kupenda kazi
(6). Kutekeleza wajibu wao.


Dhima
Kuwalea vijana wa Tanzania ili wawe na nidhamu, uzalendo na ujuzi ambao utawawezesha kushiriki kikamilifu
katika Ulinzi, Usalama pamoja na Ujenzi wa Taifa...

Nakushauri ujiunge kijana,Tanzania ya kesho ii mikononi mwenu!

mhh..nitafkiria but sidhani kama nitakwenda..nchi yenyewe hii..nimezaliwa tu hapa ila siipendi tanzania..watu wanaiendesha wanavyojua wao..
 
Flyn ryder pamoja na madudu mengi yanayotokana na nchi kukosa uongozi shupavu ila sio busara kuvunjika moyo mapema namna hiyo...Unakotamani kuna wenzio wanatamani ulipotoka,dawa ni mimi na wewe kusimama imara na baada ya kiza kuondoka tutarudishiwa nchi yetu,Nchi inayothamini utu na mshikamano wa watu wake na kuanzia hapo hata vijana wanaochipukia wataitazama Tanzania yenye kutia moyo!
 
Back
Top Bottom