Hivi utapeli wa namna hii huwa inakuwaje?

Hivi utapeli wa namna hii huwa inakuwaje?

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2017
Posts
1,579
Reaction score
3,798
Habari zenu wanaJF

Naomba msaada hapa.

Kuna rafiki yangu ana ofisi ya kutoa huduma za wakala wa fedha, kama m-pesa, halopesa na tigopesa.

Sasa anabinti amemuajili pale, jana Binti katapeliwa lakini kwa jinsi anavoelezea na kama huu utapeli una uchawi ndani yake.

Yani kuna binti mdogo kwa maelezo yake ni kama wa miaka 18-22.

Anadai kwamba huyo binti alifika pale ofisini akamsalimia yule mtoa huduma na baada ya hapo akamuomba pesa, yule mhudumu akamuliza shingap tapeli akajibu laki tano yule binti bila kupinga na kiulaini kazama kwenye droo katoa pesa tapeli kapokea akaamsha.

Baada ya muda kidogo ndo mhudumu akapata fahamu akagundua kuwa katapeliwa.
 
WaTZ mnaamini kila kitu uchawi. Kuna dawa inahusika inaitwa Scopolamine aka devil's breath. Inaadhiri sehemu moja ya ubongo ila unabaki conscious kupokea amri na kutekeleza.

Unaweza ukaambatana na mtu hadi atm machine, ukaweka pin, ukatoa hela na kumpa huyo aliyekupulizia. Huku Nairobi inatumika sana na matapeli.

Mtaenda naye hadi nyumbani kwako, umsaidie kupaki vitu vyote aondoke navyo. Senses zako zitarudi baada ya masaa kadhaa. Tafuta Scopolamine kwenye Google
 
Habari zenu wanaJF

Naomba msaada hapa.

Kuna rafiki yangu ana ofisi ya kutoa huduma za wakala wa fedha, kama m-pesa, halopesa na tigopesa...
haya mambo yapo mkuu kuna kipindi niliwahi kufanya biashara ya fedha, alikuja jamaa yuko na haraka sana aka omba niweke pale elfu ishirini nimtumie mtu wake kisha na kusepa zake nikafanya vile kwa number ya simu alio iacha pesa yake nikaweka ndani ya droo kulikuwa na milioni moja ndani yake nikaendelea na kazi muda nataka kuweka pesa kwenye simu yaan ( float ) na kuta pesa amna nilibaki nashangaa inawezekanaje pesa kupotea .
 
Habari zenu wanaJF

Naomba msaada hapa.

Kuna rafiki yangu ana ofisi ya kutoa huduma za wakala wa fedha, kama m-pesa, halopesa na tigopesa.

Sasa anabinti amemuajili pale, jana Binti katapeliwa lakini kwa jinsi anavoelezea na kama huu utapeli una uchawi ndani yake.

Yani kuna binti mdogo kwa maelezo yake ni kama wa miaka 18-22.
Anadai kwamba huyo binti alifika pale ofisini akamsalimia yule mtoa huduma na baada ya hapo akamuomba pesa, yule mhudumu akamuliza shingap tapeli akajibu laki tano yule binti bila kupinga na kiulaini kazama kwenye droo katoa pesa tapeli kapokea akaamsha.

Baada ya muda kidogo ndo mhudumu akapata fahamu akagundua kuwa katapeliwa.
Mmhhhh,
Amuulize vizuri huyo. Hakuna kitu kama hicho.
 
Nimekutumia no yangu PM..nicheki😂😂
Nimeona, expect ujumbe wangu nikishaipata kwa ajili ya majaribio.

Uje tayari tayari kupumbazwa na scopolamine😂😂

Scopolamine mixer mkongo, lazima uombe maji.
 
Back
Top Bottom