Msomi akipata shavu la kuajiriwa serikalini, inakuwa raha msarehe. Hatakiwi kuguswa hata akiiba; anahamishiwa sehemu nyingine. Hivi huu utaratibu uko kwetu Tanzania tu au ni duniani kote? Mtu unakula kodi za walalahoi, unaiba, unakosea, halafu eti usisemwe na ikiwezekana uhamishiwe sehemu nyingine uendelee kuiba kule uendako.
Tuna watu wamegraduate tangu 2015 mpaka leo hawana kazi lakini unakuta mtumishi wa umma, jizi tena limekubuhu, linaachwa au linahamishiwa sehemu nyingine. Hivi huyu mtumishi jizi akifukuzwa kazi akaajiriwa mwingine kuna shida gani?
Aisee, mimi nikiwa rais nabadilisha kila kitu. Mswada wa kwanza kupelekwa bungeni utakuwa wa kubadilisha utaratibu huu. Hatuwezi kukaa na wazembe, majizi nk maofisini, halafu eti tutegemee mabadiliko, nchi ipae kiuchumi.