Hivi utaratibu wa TRA mtu akifungua biashara anatakiwa akae muda gani bila kulipa kodi na hii kitu infanyajwe officially

ps3

Member
Joined
Nov 11, 2018
Posts
14
Reaction score
18
Wazee nimeanzisha biashara haina hata mwezi ila TRA wameshaanza usumbufu. Nilisikia kwamba kunamsamaha wa kodi kwa biashara mpya sijui ni miezi sita. Nikitaka kupewa huo msamaha officially inakuaje kwa anayejua utarabu jamani.
 
Mkuu inategemea ni biashara ipi na kuna biashara nyingine ambazo zipo kwa jina la kampuni unatakiwa kufanya makadirio mwanzo wa biashara/huduma hiyo na unalipa kabla ya kujua faida itakujaje hiyo kodi inaitwa ‘provisional tax’

Sielewi utaratibu wa hizi biashara ambazo hazipo ktk mwavuli wa ‘limited company’ je nazo unakadiria mapato yako ukianza biashara na unaanza kulipa kodi mwanzo kabisa wa biashara

Lkn hii provisional tax unakuja ku ‘claim’baadae ktk kutengeneza hesabu kama ulipata hasara ama faida , kwa hasara inakuwa umewalipa in ‘advance’bado ni yako kwa faida wanaagalia ‘total ‘faida yako wanatoa hiyo uliyolipa na huwa inalipwa kwa vipindi vinne ndani ya mwaka
 
Wazee nimeanzisha biashara haina hata mwezi ila TRA wameshaanza usumbufu. Nilisikia kwamba kunamsamaha wa kodi kwa biashara mpya sijui ni miezi sita. Nikitaka kupewa huo msamaha officially inakuaje kwa anayejua utarabu jamani.
Hili kweli lakini muda wa malipo sio miezi 6 bali ni ndani ya siku 90 (miezi 3)
Ipo hivi:
Nenda TRA katika kituo chako cha huduma za kodi kwa mteja, kama biashara unaanza utakuwa na (individual case):
1. Fomu za maombi ya TIN za kutoka TRA
2. Barua ya Mwenyekiti serikali za Mtaa ya utambulisho ambayo hutolewa pia TRA
3. Mkataba wa pango
4. Kopi ya kiambulisho na
5. Picha ya passport

Baada ya hapo utakadiriwa kodi ie provison tax kwa mwaka mzima ambayo utataakiwa kulipa ktk awamu nne ie
1. Awamu 1: mwisho kulipa 31 Machi
2. Awamu 2: mwisho kulipa 30 Juni
3. Awamu 3: mwisho kulipa 30 Septemba
4. Awamu 4: mwisho kulipa 31 Disemba

Baada ya makadirio utaomba muda zaidi wa kuangalia biashara yako ili ulipe. Hivyo utapewa siku 90, ndani ya siku hizo 90/utafanya malipo yako ya awamu ya kwanza.
(Nyongeza) Je kama biashara ipo vibaya sana, utalipa iwe awamu ya kwanza halafu utaandika barua ya kuomba marejeo ya makadirio na kujaza fomu ya makadirio upya kwa kiwango utakachoweza kulipa. Na kama biashara nzuri pia utafanya hivyo.

TUENDELEE NA SUALA LAKO
Sasa baada ya kupewa haya makadirio unaweza kuomba Certificate of Tax Clearance ili ikusaidie kupata leseni. Hapa vlvl utalazimika kulipa kodi na ushuru wa Mkataba wa pango ( usijesema mbona nalipa kodi ya makadirio ya awali, hii ni tofauti. Baada ya kulipa:
1. Kodi ya zuio (withholding tax 10% ya muda uliolipia mkataba wk)
2. Ushuru wa stempu (Stamp duty 1% ya muda uliolipiwa, huchajiwa kwa mwaka mzima ht km umelipia miezi michache)
Baada ya malipo haya utakuwa huru kupambana ndani ya siku hizo 90 kulipa awamu yao ya kwanza.
Natumaini umeelewa vema, acha na wengine waongezee zaidi
 
Mkuu hayo mambo mi yalinishinda yaan biashara nimeanza mwezi wa kumi na moja,
Ila kwenye makadirio ya kodi naambiwa nilipie 150000 kodi ya mwaka mzima wakati hicho kipindi cha nyuma sikuwa na biashara sasa vipi nilipie kitu ambacho sikuwanacho?
Nilichofanya nilichukua TIN namba yangu nikaondoka,sijarudi tena
Tutaonana january INSHAALLAH.
 
Ni kweli kn mambo yana ukakasi sana utekelezaji wake
 
Yaani hili suala la kodi hapa kwetu ni tatizo, unaanza biashara wanakukadiria mapato, unalipa hata kama hujakusanya hiyo fedha, mwaka unaofuata unakadiriwa ongezeko kubwa zaidi, mimi mwaka juzi nilikadiriwa laki 2, biashara ya stationary, mwaka huu waka nikadiria laki 8! nikawaambia silipi nikaandikambarua ya kufnga biashara hapo hapo ofisini kwao, wakaniambia unaweza kulipa nga[i nikaw waambia hata ile laki mbili nililipa hasara, eti basi toa laki tano nikawaambia pokeeni tu hii barua, nikaondoka..Ni wapuuzi some times juzi rais amesema kweli wanafilisi watu hawa TRA.
 
Jamani mimi nauliza, nimeimport daladala Mitsubishi Rosa Fuso kwa ajili ya kuzungusha sasa utaratibu unakuaje wa kuianza iyo biashara??
Nauliza kwa kuwa sioni kama iyo inahitaji jina la kampuni au bra bra nyingine kwan naiona km biashara ya taxi tu.
Naomba jibu wadau
 
Kodi ni nyingi mpaka basi ,,Mungu turehemu waja wako ,,
 
Hili kweli lakini muda wa malipo sio miezi 6 bali ni ndani ya siku 90 (miezi 3)
Ipo hivi:
Nenda TRA katika kituo chako cha huduma za kodi kwa mteja, kama biashara unaanza utakuwa na (individual case):
1. Fomu za maombi ya TIN za kutoka TRA
2. Barua ya Mwenyekiti serikali za Mtaa ya utambulisho ambayo hutolewa pia TRA
3. Mkataba wa pango
4. Kopi ya kiambulisho na
5. Picha ya passport

Baada ya hapo utakadiriwa kodi ie provison tax kwa mwaka mzima ambayo utataakiwa kulipa ktk awamu nne ie
1. Awamu 1: mwisho kulipa 31 Machi
2. Awamu 2: mwisho kulipa 30 Juni
3. Awamu 3: mwisho kulipa 30 Septemba
4. Awamu 4: mwisho kulipa 31 Disemba

Baada ya makadirio utaomba muda zaidi wa kuangalia biashara yako ili ulipe. Hivyo utapewa siku 90, ndani ya siku hizo 90/utafanya malipo yako ya awamu ya kwanza.
(Nyongeza) Je kama biashara ipo vibaya sana, utalipa iwe awamu ya kwanza halafu utaandika barua ya kuomba marejeo ya makadirio na kujaza fomu ya makadirio upya kwa kiwango utakachoweza kulipa. Na kama biashara nzuri pia utafanya hivyo.

TUENDELEE NA SUALA LAKO
Sasa baada ya kupewa haya makadirio unaweza kuomba Certificate of Tax Clearance ili ikusaidie kupata leseni. Hapa vlvl utalazimika kulipa kodi na ushuru wa Mkataba wa pango ( usijesema mbona nalipa kodi ya makadirio ya awali, hii ni tofauti. Baada ya kulipa:
1. Kodi ya zuio (withholding tax 10% ya muda uliolipia mkataba wk)
2. Ushuru wa stempu (Stamp duty 1% ya muda uliolipiwa, huchajiwa kwa mwaka mzima ht km umelipia miezi michache)
Baada ya malipo haya utakuwa huru kupambana ndani ya siku hizo 90 kulipa awamu yao ya kwanza.
Natumaini umeelewa vema, acha na wengine waongezee zaidi
Duh!
Kumbe kuanzisha biashara bongo kuna mazingira magumu hivi?
Bora kuwekeza Kenya sasa au Rwanda
 
Kiongozi, nisaidie na mimi. Nilikuwa na kibanda ambacho TRA walinikadiria kulipa kod ya sh. 150,000 kwa mwaka. Kwa sasa mauzo yameshuka hadi 25% ambapo nashindwa kumudu gharama za kulipa kodi ya mapato. Nifanyeje ili nisilipe mapato?
 
Jamani mimi nauliza, nimeimport daladala Mitsubishi Rosa Fuso kwa ajili ya kuzungusha sasa utaratibu unakuaje wa kuianza iyo biashara??
Nauliza kwa kuwa sioni kama iyo inahitaji jina la kampuni au bra bra nyingine kwan naiona km biashara ya taxi tu.
Naomba jibu wadau

Ni "blaa blaa". " braa" ni sidiria
 
Jamani mimi nauliza, nimeimport daladala Mitsubishi Rosa Fuso kwa ajili ya kuzungusha sasa utaratibu unakuaje wa kuianza iyo biashara??
Nauliza kwa kuwa sioni kama iyo inahitaji jina la kampuni au bra bra nyingine kwan naiona km biashara ya taxi tu.
Naomba jibu wadau
Wewe utakutana na
1. TRA kwenye kodi ya mapato, kama utakuwa na ofisi lazima ulipe kodi ya zuio na ushuru wa stempu wa mkataba
2. SUMATRA ktk kibali cha biashara ya usafirishaji
3. Wizara ya viwanda biashara na uwekezaji ktk leseni ya biashara
 
Yaani hili suala la kodi hapa kwetu ni tatizo, unaanza biashara wanakukadiria mapato, unalipa hata kama hujakusanya hiyo fedha, mwaka unaofuata unakadiriwa ongezeko kubwa zaidi, mimi mwaka juzi nilikadiriwa laki 2, biashara ya stationary, mwaka huu waka nikadiria laki 8! nikawaambia silipi nikaandikambarua ya kufnga biashara hapo hapo ofisini kwao, wakaniambia unaweza kulipa nga[i nikaw waambia hata ile laki mbili nililipa hasara, eti basi toa laki tano nikawaambia pokeeni tu hii barua, nikaondoka..Ni wapuuzi some times juzi rais amesema kweli wanafilisi watu hawa TRA.
Aisee pole sana. Sio siri mazingira ya biashara bongo ni ya uhasama sana.yaani hela yote inaishia serikalini
 
Kiongozi, nisaidie na mimi. Nilikuwa na kibanda ambacho TRA walinikadiria kulipa kod ya sh. 150,000 kwa mwaka. Kwa sasa mauzo yameshuka hadi 25% ambapo nashindwa kumudu gharama za kulipa kodi ya mapato. Nifanyeje ili nisilipe mapato?
Pole sana Mkuu Lihakanga
Baada ya makadiro ktk ile awamu ya kwanza ya malipo, kama biashara ilikuwa na hali mbaya kwa kushika kimauzo ulitakiwa ichukue hutua:
1. Kuandika barua juu ya hali halisi ya biashara kwa wakati huo
2. Kujaza fomu ya makadirio iliyorejewa ie revised provison tax form ambayo inaonyesha uwezo wk wa kulipa
Sasa basi
Kama mauzo unasema yameshika kwa 25% hii ina maana kuna uwezekano mkubwa wa mauzo kuwa:
Scenario 1
Mauzo yk yapo kati ya mil 4 hadi mil 6 lkn hayafiki mil 7.5 (nakisia tu coz hukisema ulikuwa wauza kiasi gani kabla. Lkn kwa kodi ya 150,000 ina maana mauzo yk yalikuwa kati ya mil 4 hadi mil 7.5. Hivyo kama "assumption" juu hp ni sawa utatakiwa kulipa kodi ya 150,000 ile ile na mwaka ujao

Scenario 2
Kama mauzo baada ya kushuka kwa 25% yapo au yanakaribia mil 4 lkn si mil 4 basi hutalipa kodi kwa mwaka ujao wa fedha

Nini ufanye
Andika barua na kuelezea kinagaubaga juu ya kishuka kwa mauzo na biashara yako pia. Ikibidi hata kuwakaribisha sehem yk ya biashara kushuhudia hilo km wanabisha
 
Nakushukuru sana mkuu, umeenda mle mle hakika. Assumption yako kama uliiona biashara yangu vile. Kwa kuwa Desemba hii nalipa installment ya mwisho, nafikiri nianze kupambana kujitetea. Asante sana kwa msaada wako.
 
Kiongozi, nisaidie na mimi. Nilikuwa na kibanda ambacho TRA walinikadiria kulipa kod ya sh. 150,000 kwa mwaka. Kwa sasa mauzo yameshuka hadi 25% ambapo nashindwa kumudu gharama za kulipa kodi ya mapato. Nifanyeje ili nisilipe mapato?
Kachukue kitambulisho cha machinga tuu mkuu. Elfu 20 tu husumbuliwi tena na mtu
 
Hili kweli lakini muda wa malipo sio miezi 6 bali ni ndani ya siku 90 (miezi 3)
Ipo hivi:
Nenda TRA katika kituo chako cha huduma za kodi kwa mteja, kama biashara unaanza utakuwa na (individual case):
1. Fomu za maombi ya TIN za kutoka TRA
2. Barua ya Mwenyekiti serikali za Mtaa ya utambulisho ambayo hutolewa pia TRA
3. Mkataba wa pango
4. Kopi ya kiambulisho na
5. Picha ya passport

Baada ya hapo utakadiriwa kodi ie provison tax kwa mwaka mzima ambayo utataakiwa kulipa ktk awamu nne ie
1. Awamu 1: mwisho kulipa 31 Machi
2. Awamu 2: mwisho kulipa 30 Juni
3. Awamu 3: mwisho kulipa 30 Septemba
4. Awamu 4: mwisho kulipa 31 Disemba

Baada ya makadirio utaomba muda zaidi wa kuangalia biashara yako ili ulipe. Hivyo utapewa siku 90, ndani ya siku hizo 90/utafanya malipo yako ya awamu ya kwanza.
(Nyongeza) Je kama biashara ipo vibaya sana, utalipa iwe awamu ya kwanza halafu utaandika barua ya kuomba marejeo ya makadirio na kujaza fomu ya makadirio upya kwa kiwango utakachoweza kulipa. Na kama biashara nzuri pia utafanya hivyo.

TUENDELEE NA SUALA LAKO
Sasa baada ya kupewa haya makadirio unaweza kuomba Certificate of Tax Clearance ili ikusaidie kupata leseni. Hapa vlvl utalazimika kulipa kodi na ushuru wa Mkataba wa pango ( usijesema mbona nalipa kodi ya makadirio ya awali, hii ni tofauti. Baada ya kulipa:
1. Kodi ya zuio (withholding tax 10% ya muda uliolipia mkataba wk)
2. Ushuru wa stempu (Stamp duty 1% ya muda uliolipiwa, huchajiwa kwa mwaka mzima ht km umelipia miezi michache)
Baada ya malipo haya utakuwa huru kupambana ndani ya siku hizo 90 kulipa awamu yao ya kwanza.
Natumaini umeelewa vema, acha na wengine waongezee zaidi
Mkuu kama Flem au jengo ni lako inakuaje hapo kwenye mkataba wa pango?
 
Back
Top Bottom