Hivi uzalendo ni kuwapunguzia Watu mlo, na si kinyume chake?

Hivi uzalendo ni kuwapunguzia Watu mlo, na si kinyume chake?

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Kiongozi anapambana kuaminisha Watu kuwa tunahitaji kupunguza matumizi/lishe ili tukidhi vigezo vya Uzalendo, hii ni sawa? sio kwamba tunatakiwa tuongeze kipato ili tule vizuri...Yaani badala ya kula vipande vitatu vya mihogo sasa tunatakiwa tule kipande kimoja tu au hata tushindie maji?

Siku zote Mwenye shibe hawezi kukuelewa wewe Mtu unayelia njaa maana yeye haijui njaa...wao na familia zao wanachagua chakula wanachohitaji kwa siku ili hali Wenzao huko wanakula kinachopatikana.

Hivi wanajua tunavyowatumia pesa Wapendwa wetu Vijijini kuiachia elfu tano nzima inauma kiasi gani? hiyo 5000 ingemsaidia mambo mangapi? kwa kuwa wao hawaiwazii hiyo 5000 ni rahisi tu kutuita Walalamishi.

Hizi akili za kuangalia upande mmoja tu wa shilingi na kuacha kwingine sijui ni akili za wapi?...huenda kweli kuna kina Diamond hawapungukiwi chochote kukatwa hata 50000 kwa miamala, sasa vipi Bibi na Babu wa kule Namanyere anayeambulia 5000 tu baada ya kum beep wiki nzima Mwanaye Mmachinga wa huku Moshi Mjini? nao tunawalisha kauli hizohizo ya uzalendo wakati tayari anapambana na utapia mlo?

Wakati tunatakiwa kuwahimiza Wananchi wetu kula vizuri, kunywa Maziwa walau kila siku, Nyama na Mayai sisi ndio kwanza tunawaza kuwapunguzia kipato ili tu wajiite Wazalendo. Kwa hiyo tutarajie makubwa kutoka taifa la Wenye lishe duni ndio wajenge viwanda au wabuni teknolojia za kushindana na wengine?. sio kwamba sisi tutabaki wa kutengenezewa tu na kuletewa kila kitu mpaka mwisho wa dunia?

Huko kwa Wenzetu wanaamini kwenye lishe bora kwa Wananchi wao ndio waweze kuwa na akili na kuwa Wabunifu na wenye maaraifa zaidi...sisi huku wa Dunia ya tatu kila kukicha tunawaza kupunguziana vipato ndio tujiite Wazalendo.

Bila kuandaa taifa la Wenye akili tutabaki na taifa la Wafunga mkanda mpaka mwisho wa Dunia.
 
Mzee mgaya 1978-2021
Nikufunga mikanda
Tuambiwe mikanda mingapi Imeshabadilishwa?
Viuno havijachubuka tu
 
Hata wasiojulikana walipata kuitwa wazarendo tena kweli kweli, ni maajabu yanayopatikana tz pekee.
 
Back
Top Bottom