Red Giant
JF-Expert Member
- Mar 9, 2012
- 15,657
- 20,967
- Thread starter
- #21
shukrani sana. nimekupata vyema.Hiyo bidhaa ya TZS 100,000 kama umenunua kwa mfanyabiashara aliyesajiliwa tayari ndani yake kuna VAT TZS 15,254.
Endapo umeuza TZS 120,000 ikijumuisha VAT, VAT hapo ni TZS 18,305.
Utakacholipa TRA ni TZS 3,051 hii ndio kodi ya Ongezeko la thamani kati ya bei uliyouzia na ile uliyonunulia.
Ugumu kwenye VAT unakuja pale unaponunua kwa mtu ambaye hakusajiliwa VAT wakati wewe umesajiliwa VAT. Ili usipate shinda kwenye sheria ya VAT, kama wewe umesajiliwa VAT nunua bidhaa zako kwa mtu aliyesajiliwa VAT kwani ile VAT unayolipa kwenye manunuzi si gharama ya biashara yako, utajirudisha kwa kupunguza kwenye VAT uliyowatoza wateja wako.