shukrani sana. nimekupata vyema.Hiyo bidhaa ya TZS 100,000 kama umenunua kwa mfanyabiashara aliyesajiliwa tayari ndani yake kuna VAT TZS 15,254.
Endapo umeuza TZS 120,000 ikijumuisha VAT, VAT hapo ni TZS 18,305.
Utakacholipa TRA ni TZS 3,051 hii ndio kodi ya Ongezeko la thamani kati ya bei uliyouzia na ile uliyonunulia.
Ugumu kwenye VAT unakuja pale unaponunua kwa mtu ambaye hakusajiliwa VAT wakati wewe umesajiliwa VAT. Ili usipate shinda kwenye sheria ya VAT, kama wewe umesajiliwa VAT nunua bidhaa zako kwa mtu aliyesajiliwa VAT kwani ile VAT unayolipa kwenye manunuzi si gharama ya biashara yako, utajirudisha kwa kupunguza kwenye VAT uliyowatoza wateja wako.
Hizo claim ni siasa tu,cjui hata kama watalipainput itakuwa 18000 na output 21600. kwa hiyo ntalipa 3,600? ni ikitokea nimeuza kwa hasara labda 90,000 na VAT ikawa 16200 inabidi niende TRA kudai (16200-18000) 1,800?. nafikiri nimekupata.
Mkuu na ukiclaim refund wanakurudishia kwa mtindo gani?Mfano upo hivi
(1)Umenunua bidhaa 100,000
Jumlisha Vat 18%=18,000
Kwa hiyo jumla bidhaa umeinunua kwa 118,000
(2) Bidhaa unaiuza kwa 150,000 vat exclusive
Jumlisha vat 18%=27000
Kwa hiyo bei ya bidhaa itakuwa sh.177,000 vat inclusive
Ukicheki hiyo mifano miwili hapo juu;
Vat ilichajiwa mfano A ni Input tax (vat on purchase)
Vat iliyochajiwa mfano B ni Output tax(vat on sales)
Sasa ikitokea Output tax ni kubwa kuliko input tax tofauti unaenda kulipa Tra
Mfano:27,000-18,000=9,000
Na ikitokea Input tax ni kubwa kuliko Output tax tofauti ni refund/claim (Tra wanapaswa kukurudishia)
Credit kwenye future taxes utakazolipa. Hurudishiwi cash. Never.Mkuu na ukiclaim refund wanakurudishia kwa mtindo gani?
Ok kamanda... thanksCredit kwenye future taxes utakazolipa. Hurudishiwi cash. Never.
Kwa hiyo tra watakupa pesa hiyo kweli?input itakuwa 18000 na output 21600. kwa hiyo ntalipa 3,600? ni ikitokea nimeuza kwa hasara labda 90,000 na VAT ikawa 16200 inabidi niende TRA kudai (16200-18000) 1,800?. nafikiri nimekupata.
huja soma.SheriaMfano nimenunua bidhaa 100,000, nikiweka gharama zingine inafika 103,000 na nimeuza bidhaa hiyo 120,000 na kupata faida 17,000.
Je, VAT itakuwa 18% ya 120,000, yaani 21,600?.
Au itakuwa 18% ya 17,000 yaani 3,060?
Sheria ya kodi ya nchi inasemaje kuhusu VAT?
Nchi zingine zinafanyaje?
Naomba kujuzwa.
Biashara sio duka tu. Mfano una garage VAT registered, mara nyingi unanunua parts in retail kutokana na demand ya siku hio. Obviously utanunua kwa retailer ambao wengi sio vat registered.
Nyinginezo kasoro VAT. Mfano mapato,corparate tax,withholding tax etc. Wenye maduka wanakadiriwa kodi ya mwaka.Muuzaji asiyesajiliwa VAT hulipa kodi gani mbadala wa VAT?