Nguo ya ndani yoyote, iwe chupi, fulana au sidiria kazi kuu ni kukinga nguo za nje zisichafuke kwa maji maji yanayotolewa na mwili, kibailojia km jasho, mkojo, shahawa, damu ya hezi, kinyesi, nk.
Sababu nyingine, km chupi husaidia kulinda heshima ya mtu kwa kuhifadhi sehemu za siri vizuri km mwanaume ambaye uume wake utasisimka kwa sababu mbalimbali mbele ya kadamnasi ya watu.
Lakini pia kuna hasara za kiafya kuvaa chupi ikiwa ni pamoja na kujiambukiza magonjwa ya sehemu za siri, kama chupi hazibadilishwi mara kwa mara na mvai mgonjwa.