Hivi viatu vya 3000 huwa vinatoka wapi? Nataka niingie kwenye biashara ya viatu

Hivi viatu vya 3000 huwa vinatoka wapi? Nataka niingie kwenye biashara ya viatu

toplemon

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2017
Posts
4,612
Reaction score
4,721
Ni alhamis tamu sana kukiwa na hali ya hewa ya mawingu na ubaridi na kimvua hapa dar hakika napendaga hii hali sana.

Ok niende kwenye mada unaweza ukapita mahali au kwenye masoko hapa dar unakuta viatu vinauzwa 3000 mpaka 4000 ni viatu vizuri sana mimi siku zote nimekua na ndoto ya kufanya biashara ya viatu vya mtumba kama hivyo ila nashindwa kujua ni wapi wanavitoaga niliuliza mmoja akaishia kutabasamu tu hakunambia chochote.

Naombeni mnishauri juu ya hili pia ningependa kujuwa ni wapi nitapata hivyo viatu namaanisha chimbo la hivyo viatu ili nami nianze na hii biashara Na hata pia bei zinakuaje.

Natumai nitapata mwongozo!
 
Nijuavyo ni kwmba, ukinunua balo la viatu mitumba mule ndani unapata viatu vya grade tofauti tofauti kuanzia vizuri sana hadi vibaya kabisa, sasa unasort viatu vyako vizuri umapanga bei kubwa kisha unaendelea hivyo mpaka unakamilisha idadi yako na makadirio yafaida then viatu vinavyobaki visivyo na ubora sana unaviuza kwa bei chini ndio hivyo unavosema vya elfu 3 na 4.

Asante
 
Balo shi ngap?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kuanza usinunue bello unaweza ukakata mtaji....we anza na viatu vya kupoint....nenda soko la karume ilala asubuhi sana ndio wanafungua mabello... chagua viatu vyako Nenda kavioshe vizuri au piga kiwi...tayari kwa kuuza.
 
Amka asubuhi na mapema wahi karume, kunakua na mnada. Wananunua kwenye mnada asubuhi kisha wanaenda viosha kama ni vya shule wanapiga dai na kiwi mzigo unaingia sokoni.
 
kwa kuanza usinunue bello unaweza ukakata mtaji....we anza na viatu vya kupoint....nenda soko la karume ilala asubuhi sana ndio wanafungua mabello... chagua viatu vyako Nenda kavioshe vizuri au piga kiwi...tayari kwa kuuza.
Muda wa kuanzia saa ngap hyo asubuh
 
Amka asubuhi na mapema wahi karume, kunakua na mnada. Wananunua kwenye mnada asubuhi kisha wanaenda viosha kama ni vya shule wanapiga dai na kiwi mzigo unaingia sokoni.
Muda kuanzia saa ngap hyo asubuh
 
Ukitaka kupata mzigo hakikisha saa 10 kamili inakukuta upo karume au ilala

Panga mwenyewe utatoka saa ngapi unapokaa ili 10 kamili ikukute eneo husika

Saa 11 tayari pashachangamka na viatu vikali vishawahiwa na wajanja ambaoo saa 9 wapo macho.
 
Hadi saa 1 wanafungua lakini uwe na nguvu za kutosha tu maana ni full ngumi kwenye kugombania mie nliendaga nkaishia kupata hasira tu maana kuna watu wanajifanya soko kama la baba yao full kilichotokea kuna mmoja akajichangsnya akachezea kelbu za kutosha nkasepa zangu mpka leo sna hamu napo
 
Full information inakurahshia mtu kupata kile unachohtaj kwa muda sahih
Isifike saa 12 asubuhi ukiwa unakagua. Inabidi ujue unataka vya shilingi ngapi jumla hivo utatumia jumla ya muda gani. Naamini huna experience na Karume kama umeuliza swali hili. Muda wa kufika iwe mapema saa 10 hivi.
 
hadi saa 1 wanafungua lakini uwe na nguvu za kutosha tu maana ni full ngumi kwenye kugombania mie nliendaga nkaishia kupata hasira tu maana kuna watu wanajifanya soko kama la baba yao full kilichotokea kuna mmoja akajichangsnya akachezea kelbu za kutosha nkasepa zangu mpka leo sna hamu napo

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku tulikurupuka na mshikaji wangu tufanye biashara ya samaki Nyumba ya Mungu Kilimanjaro. Kumbe kile kipindi samaki ni adimu kinoma,wavuvi wakirudi ile mida ya saa nane usiku kama huna nguvu huambulii kitu. Tulienda na mindoo kama minne hivi,tulichoambulia ni robo ndoo halafu tumezinguana na watu huo usiku,mikono imevimba kwa kuchomwa na miba ya samaki,tumelowa chepe chepe kwa kuwa ilikuwa kipindi cha mvua. Hapo nilikuja gundua theories za evolution kama IN THIS WORLD ONLY THE STRONG SURVIVE ni ukweli
 
kwa kuanza usinunue bello unaweza ukakata mtaji....we anza na viatu vya kupoint....nenda soko la karume ilala asubuhi sana ndio wanafungua mabello... chagua viatu vyako Nenda kavioshe vizuri au piga kiwi...tayari kwa kuuza.
Asante sana mkuu....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom