Hivi video za wasanii wetu zinaitangazaje nchi yetu?

SAUTI YAKO

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2014
Posts
2,944
Reaction score
2,032
Wadau wa muziki, ninashangazwa sana na hawa wasanii wetu wa bongo fleva ambao wanashindwa kuitangaza nchi yetu na kuamua kila video yao mpya kwenda kuifanya South Africa utadhani huko ndio nyumbani kwao.

Hivi Tanzania yetu haina maeneo mazuri yanaofaa kwa location mpaka kila video iwe ni nje tu hasa South Africa? Zanzibar mbona kunavutia.

Kama ishu ni watengenezaji bora wa video kwanini msiwaite waje hapa nchini?
Nani atatangaza vivutio tulivyonavyo kama sio video zenu?

Jamani kama majumba makali hapa yapo, mahotel makali yapo, tatizo nini?

Mkataa kwao ni mtumwa!
 
Nadhani hawafuati location, wanafuata ubora wa video na majina makubwa ya makampuni ya uandaaji wa video. Pia kuwaleta hao watu bongo inavyoonekana ni gharama sana, so kupunguza gharama wanaona bora waende tu.
 
South wengi wao wanafuata ma Directors na connection. Huwezi kusema msanii alazimike kumgharamia Director, Editor, n.k pesa ya nauli, malazi ili aje kushoot bongo itakuwa ni gharama kubwa sana..

Afu kingine hizo uvyosema vivutio, kufanya shooting huko ni gharama afu inachukua mlolongo mrefu sana kufanikisha ishu nzima, wakati South Africa ni rahisi sana kupata location unazotaka. Chukulia mfano lile Daraja waliloshoot kwenye Bado ya harmonize walitumia muda wa nusu saa huku gari zote zimezuiliwa, sasa jiulize unaweza kufanya hicho kitu kwenye Daraja la Kigamboni? tena bure?
 
Kaziya kutangaza nchi ni kazi ya bodi ya Utalii na wanalipwa mshahara kwa sababu hiyo na badget wanapewa, sasa wewe unataka wasanii wafanye kazi bure wakati wana makampuni yao ambayo mwisho wa mwezi mnayadai kodi ?
 
Watanzania ni lini tutaacha hii kasumba ati wasanii "kutangaza vivutio"??

Hivi msanii akitoa nyimbo nzuri na video kali ikatikisa Afrika, hajaitangaza nchi hapo??

Alafu muziki ni biashara! Watu wanenda SA kwasababu ngingi.. Quality za video, na ni rahisi kupata access ya location.. Hapa bongo kwa mfano utake kufunga barabara ili ushoot video mpaka upewe kibali ni miezi kadhaa labda..
Pia directors wa SA wanaconnectios na vituo vya TV vya kimataifa..

Acheni wasanii waende SA na ikiwezekana hata USA wakatengeneze video Kali.. Wanajiweka kwenye nafasi nzuri ya kujipatia mafanikio binafsi, wanakuza mziki na wanaitangaza nchi..
 
Zanzibar? Usithubutu kupeleka makalio wazi kule kwa ajiri ya video. Wale watu wakuda lazima walete kwere.
 
Mnalalamika nchi itangazwe wakija watu wa kikatiwa viunga kgambon mnasema wazawa hatendew hak
 

[emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka sana love...sana.
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] nimecheka sana love...sana.
[emoji4] [emoji1] [emoji23]

Watu wanaishi Tanzania ila nahisi hawajui TANAPA kitu gani.. Wakimuona Sheta wanajiuliza "huyo sijui ndio Tanapa mwenyewe"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…