CreativityCode
Senior Member
- Aug 8, 2020
- 158
- 653
Shalom kutoka Jerusalem,
Mara nyingi kunapotokea sintofahamu inayohitaji uwajibikaji wa serikali viongozi wa juu wamekuwa wakiwaambia wananchi kuwa "serikali ilikuwa na nia njema kabisa". Hivi wewe mdau wa JamiiForums huwa unaelewa nini kuhusu kauli hii?
MFANO: Hivi karibuni, Tanzania, Afrika na Dunia watu wengi walisubiri kutazama moja ya Derby kubwa zaidi duniani, yaani mtanange wa miamba ya Soka yenye makazi yake Kariakoo, jijini Dar es Salaam, Simba dhidi ya Yanga, walipigwa na butwaa baada ya taarifa kutoka kwamba mechi ingesogezwa mbele kwa masaa 2 bila sababu ya msingi kuwekwa wazi, baadaye mechi hiyo iliahirishwa kabisha.
Kilichofuata ni viongozi wa serikali kutoka hadharani na kuomba msamaha bila kuweka wazi sababu hasa iliyopelekea kuahirishwa mechi husika. Yaani wanataka kusamehewa lakini hawasemi kosa lao.
Pia wanasema serikali ilikuwa na nia njema kabisa.
MIMI HUWA NAJIULIZA SANA IKIWA KIONGOZI ANASEMA "SERIKALI ILIKUWA NA NIA NJEMA KABISA" JE, INAMAANISHA KUNA WAKATI;
SERIKALI HUWA NA NIA MBAYA/OVU DHIDI YA RAIA WAKE?
NDUGU ZANGU NAOMBA MNIWEKE SAWA KATIKA HILI