Hivi Vodacom mnatuonaje kwa huu utapeli mnaojaribu kufanyia?

Hivi Vodacom mnatuonaje kwa huu utapeli mnaojaribu kufanyia?

OleWako

Member
Joined
Sep 7, 2021
Posts
25
Reaction score
73
Leo nilinunua kifurushi cha intaneti kwa njia ya mpesa. Muamala ukatoka freshi, intaneti ikashika.

Ghafla nikaletewa ujumbe ukisema salio langu halitoshi nichukue mkopo wa Tsh. elfu 4!🤔🤔

Bahati nzuri nilicheki salio langu kabla sijaendelea, na lilikuwepo la kutosha!

Utaratibu huu ni halali kweli? Kumpotosha mteja akope na kulipa huduma ambayo hana mahitaji nayo?
 
Back
Top Bottom