Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,171
WAGOMBEA kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini, wamejitokeza katika ofisi za Tume ya Uchaguzi, Manispaa ya Kinondoni kwa ajili ya kuchukua fomu za kugombea ubunge.
Wagombea 31 walifika katika ofisi hizo, huku wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakiingia kwa shamrashamara na mbwembwe huku wa upinzani wakiingia na kutoka kimyakimya.
Mgombea wa Jimbo la Ubungo kupitia CCM Hawa Ng'humbi aliwasili katika ofisi hizo saa 8:00 mchana kwa msafara wa gari 10 ambazo zilikuwa zimebeba wapembe zaidi ya 100
Baada ya kuchukua fomu huku akiwa amezungukwa na umati wa watu, aliwaambia wakazi wa Ubungo kwamba atafanya atasaidia kuondoa tatizo la maji na miundombinu katika jimbo hilo, endapo atachaguliwa kuwa mbunge.
Katika Jimbo hilo, wagombea wengine waliojitokeza ni John Mnyika wa (Chadema), Hamisi Hamad (APPT- Maendeleo), Rajabu Isumail (DP),Samira Lakhan (Jahazi Asilia,Rachel Balama (NRA),Mark Kibogoyo (SAU), Zabron Mazengo (UDP),Kamana Masoud (UMD), Naomi William (UPDP) na Julius Majaliwa (CUF).
Hekaheka hizo pia zilikuwa katika Jimbo la Kawe ambako mbunge viti maalumu aliyemaliza muda wake Halima Mdee alifika kuchukua fomu na kueleza kuwa sera yake kuu ni ardhi.
Mdee alibainisha kuwa anachukua fomu hiyo akiwa na mambo tisa ya kuyafanyika kazi endapo atachaguliwa kuwa mbunge wa Jimbo la Kawe.
Katika jimbo hilo, Angel Kizigha anayewania nafasi hiyo kupitia CCM alifika katika ofisi hizo saa 7:00 mchana na kufafanua kuwa atashirikiana na wakazi wa Kawe na kwamba wategemea utendaji bora.
Wagombea wengine waliochukua fomu katia jimbo hilo ni Nathaniel Mlaki (APPT-Maendeleo), Shaban Mapeyo (CUF), James Mbatia(NCCR-Mageuzi), Marko Benard (SAU), Grace Mohamed (UDP), Abdallah Tumbo (UMD) na Richad Pius (UPDP).
Katika Jimbo la Kinondoni nako hali ilikuwa shamrashamra ambako Mbunge anayemaliza muda wake Idd Azzan alifika katika ofisi hizo na kuchukua fomu huku akiwataka wakazi wa Kinondoni kutimiza haki yao kwa kuchagua viongozi bora kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Kwa upenda wake mgombea ubunge kupitia Chadema Philip Mogendai alisema amekwenda kulikomboa jimbo hilo katika tatizo la muda mrefu la maji.
Wagombea wengine walioochukua fomu katika jimbo hilo ni Fitina Mohamed (APPT Maendeleo),Alhaj Shaban Nassoro (CUF), Athanas Solamon (DP), Masumbuko Kassim (Jahazi Asilia), Asia Mnyumba (NRA), Aikamlee Kayumbo (UDP),Mery Osward (UMD) na David Daudi (UPDP).
My take:
Hivyo vyama (highlighted) mbona huwa havisikiki uchaguzi ukiisha, sasa naanza kuamini ile allegation ya kwamba CCM huwa inasponsa baadhi ya vyama kwa ajili ya kuua upinzani!