Cesar Saint
JF-Expert Member
- Nov 18, 2016
- 423
- 726
- Thread starter
- #21
1. Kwanini serikali ya CCM haitoi nafasi sawa kwa vyama vya upinzani katika ulingo wa siasa?
2. Ni viongozi wangapi waliotoka Chadema na wamefanya kazi nzuri katika serikali ya CCM. Mfano Dr Slaa, Juliana Shona, Mwampamba (aliharibu tu kumpenda mke wa mkubwa[emoji23])
3. Nguvu watuya Chadema umeiona mwenyewe uwanja I J3,na pale wengi waliogopa kufika kwa vitisho vya polisi.
Sky nitakupa majibu mawili ya kufikilisha kidogo.
Kwanza swala la nafasi sawa kwenye ulingo wa siasa hilo halipo duniani kote bali mtu au chama hupewa nafasi kwa kadri ya uwezo,ushawishi,nguvu na kujipambanua kwake na hii kwa lugha rahisi inaitwa “EQUITY” there is no equality in politics rather than “EQUITY”
Swala la pili mimi ni miongoni mwa watu niliofika AirPort na niseme hivi CDM haitumii rasilimali watu vizuri ni wakati wa vyama hivi vya upinzani kuacha kutumia MOB PSYCHOLOGY na zaidi vipandikize mbegu ya kiitikadi na uelewa juu ya sayansi ya siasa na uongozi kwa wanachama wake na wafuasi wake ndio kitapata matokeo kwa mtaji wa watu .
Nakupa mfano mdogo unajua kwanini CDM na vyama vya upinzani vilishinda sehemu kubwa ya majimbo Dar es Salaam na hata kiti cha uraisi? Jibu ni kuwa mwaka 2015 nguvu kubwa iliwekezwa DSM na matokeo uliyaona na hivi ndio walitakiwa kufanya .