Uchaguzi 2020 Hivi Vyama vya Upinzani Tanzania viko serious na kuongoza Serikali?


Sky nitakupa majibu mawili ya kufikilisha kidogo.
Kwanza swala la nafasi sawa kwenye ulingo wa siasa hilo halipo duniani kote bali mtu au chama hupewa nafasi kwa kadri ya uwezo,ushawishi,nguvu na kujipambanua kwake na hii kwa lugha rahisi inaitwa “EQUITY” there is no equality in politics rather than “EQUITY”

Swala la pili mimi ni miongoni mwa watu niliofika AirPort na niseme hivi CDM haitumii rasilimali watu vizuri ni wakati wa vyama hivi vya upinzani kuacha kutumia MOB PSYCHOLOGY na zaidi vipandikize mbegu ya kiitikadi na uelewa juu ya sayansi ya siasa na uongozi kwa wanachama wake na wafuasi wake ndio kitapata matokeo kwa mtaji wa watu .

Nakupa mfano mdogo unajua kwanini CDM na vyama vya upinzani vilishinda sehemu kubwa ya majimbo Dar es Salaam na hata kiti cha uraisi? Jibu ni kuwa mwaka 2015 nguvu kubwa iliwekezwa DSM na matokeo uliyaona na hivi ndio walitakiwa kufanya .
 
Siku zote WATU wanapenda KITONGAAAAAA.

Ndio maana huoni watu wakijiunga CHAUMMA au SAU au APPT Maendeleo. watu watajiunga CCM, CHADEMA, ACT ,nk

Yaani wewe pambana mwenyewe chama kikianza kuonesha mwelekeo tayari kina Pascal Mayalla watakuja kwa mbio zote kupata wanachotaka.

Hata hao unaowaona wako CCM, ikitokea leo CHAUMMA ikaingiza madarakani 98& wote watahamia CHAUMMA.

Na hivyo kwakuwa wanajua ukiwa mgombea wa CCM unashindishwa kwa nguvu ndio maana ni wachache wanachukua njia, kupambana.

Ishtoshe CCM wana orodha ya RUSHWA kama PESA mavyeo ya KUTEULIWA n.k
 
👏👏👏
 
Kiukweli CCM inawazidi vyama vya upinzani mkakati wa kifedha,Maandalizi ya kimkakati kiuchaguzi (uliona 2015
.

CCM inawazidi wengine pamoja na

A) Makada wa ccm kuongoza/na kuhozi taasisi muhimu za kiserikali hivyo kuibeba ccm kwa hali na mali.

1. Msajiri wa vyama..... yeye kuegamia ccm, biased na muda wote anafikiria kuadhibu wapinzani

2. Polisi, kutwa kucha kupambana na wapinzani

3. Majaji na mahakimu kuhukumu na kushughulikia wapinzani kisiasa.... mifano mingi watu kunyimwa dhamana, kesi haziishi nk

4. Vyombo vya ulinzi kuipa supports ccm kwa kila hali na uwezo wote.

5. Wakuu na watendaji, Mikoa, wilaya, tarafa, kata, na vijiji .... wote hawa hutenda kwa kupewa maelekezo kiccm mfano uchaguzi wa serikali za mitaa uliopita.

B) Tume huru ya uchaguzi
Endapo tunaamini katika haki na utendaji katika weledi. Nini kinazuwia kupata tume huru ya uchaguzi? Ili tuone hicho kinachosemwa "upinzani dhaifu "

Kama ccm anaamini inanguvu na haiogopi kuondolewa vipi inafanya uchaguzi na kulazimisha bila Tume huru? Kuna nini nyuma ya pazia?

C) Katiba mpya.
Tumeshuhudia kwa hofu kubwa ccm ikiharibu mchakato wa kupata katiba mpya kwa nguvu zote

Baada ya Tume ya Jaji Joseph Sinde Warioba kufanya kazi nzuri sana na yenye weledi akiwa na marehem Mwanasheria Nguli enzi za uhai wake Dr. Sengondo Mvungi kukusanya maoni ya watanzania nchi nzima na kuaanda Rasimu bora kabisa ya katiba mpya, ccm ikaona tishio

1. Ccm ikajaza wajumbe kuipanguwa rasimu na kuivuruga kabisa. Kuchomoa mawazo ya watanzania na kuchomeka yakiccm. Mzee S. Sita alihusika sana na akina mzee bulembo.

2. Haikutosha kuivuruga rasimu bora ya Jaji Warioba, mchakato ukasitishwa...... hofu yanini? Kama ccm madhubuti?

3. Sasa hivi hata hiyo iliyochafuliwa imefichwa kabisa kabatini wala haieleweki tena nini hatima yake.

Fedha na rasilimali watu pia muda vimetumika kwa gharama kubwa lakini Rasimu haijulikani ipo wapi.

D) vyama vipate mizania sawa katika kufanya siasa. Sioni ccm ikiruhusu uwanja huru kisiasa. Nimarufuku, kamata weka ndani, piga nk.

Je kwa maelezo hayo

1. Bado tunadhani wapinzani dhaifu?

2. Nikweli ccm dhaifu na inahofu? Kama sivo
A) wasitumie vyombo vya dola
B) tupate TUME HURU
C) tupate Katiba bora kupitia RASIMU BORA YA JAJI WARIOBA sio iliyochakachuliwa

Ndugu wapinzani wananguvu, weledi na wanajielewa. Tatizo hujatathmini mazingira halisi ya kisiasa Tanzania.
 
Haki ikitumika ccm haishindi uchaguzi hilo linajulikana tangu 1995.
 
Nadhani majibu umeyapata kwenye kura za maoni. Je kuna haja ya kufanya uchaguzi wa wabunge na madiwani pia?
 
Huo ni upande mmoja na upande wa pili ni je usipokuwa na mgombea urais, wananchi watakuuliza, hivi tukichagua mbunge wa chama chako na huna rais utaleta maendeleo wakati rais ndiye mwenye kila kitu?
Hupaswi kujipanga kushindwa au kuwa mpinzani au eti serikali ya mseto, hayo yote hujitokeza baada ya uchaguzi, Chama cha siasa lengo lake ni kuingia ikulu na ikulu anaingia rais si wabunge; chama cha siasa kisicho na malengo hayo kinapaswa kupewa jina lingine
 
CCM huwa na maandalizi ya kuiba kura, na wakiisha kuiba kura wanaenda kuiba kodi zetu na wakiisha kuiba kodi zetu rais anarudi kwenye kipaza sauti 😀 😀 anatutangazia watanzania kuwa anainyoosha nchi iliyoharibiwa na mabeberu 😂😂

CCM Mungu anawaona endelea kubwabwaja hapa kuwa wapinzani hawawezi kitu lkn ujue pia wahenga walisema "kila lenye mwanzo lina mwisho wake"
CCM haiwezi kudumu maana mbumbumbu wanazidi kuisha na mikakati ya kuitoa CCM madarakani ipo pale pale time will tell
 
1. Kwanini serikali ya CCM haitoi nafasi sawa kwa vyama vya upinzani katika ulingo wa siasa?
Pengine ni tatizo la ujumla kwa wananchi walio wengi (si wote), ufahamu wa uwepo wa demokrasia, usawa wa kufanya siasa na balanced political environment katika bunge havijafahamika umuhimu wake.

Wengi bado wanaona kama siasa ni itikadi fulani au ushindani wake ni sawa na ule wa Simba na Yanga. Sidhani kama hata wananchi wanajadili uchumi na maendeleo wakielekea kwenye visanduku vya kura.
 
Wafuasi wa vyama vya upinzani tu hawashauriki. Angalia comment zao.

Sasa kama wafuasi hawashauriki ndiyo uwashauri viongozi wao?
 
Tatizo la kwanza wananchi hawafahamu elimu ya uraia. Kuwafundisha hili huko vijijini inahitaji mkakati kwani sasa hivi tuna namba kubwa ya watuwazima wasiojua kusoma na kuandika.
 
Wafuasi wa vyama vya upinzani tu hawashauriki. Angalia comment zao.

Sasa kama wafuasi hawashauriki ndiyo uwashauri viongozi wao?

Ushauri upi Muheshimiwa wakutofanya siasa, kutokosoa, kutotangaza sera, kutofanya yakikatiba na kisheria!

Watu wanavunjwa miguu

Watu wanavunjwa mikono

Watu wanapotea hovyohovyo

Watu wanawekwa vizuizini

Watu wanasambaratishwa iwe vikao vya barazani, sebureni au chumbani

Watu wanazushiwa ndani na nje ya bunge

Watu wanavurugwa kwa nguvu na gharama kubwa

Wewe Mtanzania wa wapi usieona shuruba, madhira na mibinyo waipatayo wapinzani!!!!!!!

Tuweke akili na busara japo kidogo.
 
Wewe upo CCM,dont let what Chadema does sweat you!

What Chadema does is their business,not yours!

Wakiwa wanapatia au wanafeli ni wao,wewe unaharisha nini?

Hii dunia kuna wanafiki sana!
 
Tatizo la kwanza wananchi hawafahamu elimu ya uraia. Kuwafindisha hili huko vijijini inahitaji mkakati kwani sasa hivi tuna namba kubwa ya watuwazima wasiojua kusoma na kuandika.

Nikweli lakini

1. Fursa ya awali hutolewa na serikali mashuleni, vyuoni nk
-Uvccm kufanya siasa na uelimishaji popote ruksa wapinzani malfuku

2. Fursa ya pili hutolewa na serikali kuruhusu mijadala na midahalo kisiasa, kiuchumi nk. Malfuku kwa wanasiasa kufanya mijadala ilikujenga hoja yakinifu na kinzani kuelekea, demokrasia ya kweli, katiba na haki za kiraia. Wahusika ni vyama vya siasa, wanachama na wananchi kwa ujumla. Malfuku.... isipokuwa ccm ruksa

Kwa mantiki hii hiyo elimu ya haki za msingi za kiraia inapatikana vipi? Isipokuwa za ccm tu.
 
Vyama vya siasa huwa vinaongoza serikali au vinachukua serikali kuongoza nchi?
 
Lissu amejibu jana bandiko lako la kasi ya Magufuli...hata Wajerumani walijenga infrastructures
 

aiseee we jamaa nmefuatiliaga sana threads zako, kwa kutabiri tu uko vizuri! good work
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…