Hivi vyuma havijakaza hata kwa wachaga?

Hivi vyuma havijakaza hata kwa wachaga?

shinyangakwetu

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2015
Posts
2,487
Reaction score
2,394
Watu wanasema vyuma vimekaza huku wenzetu wakihama miji kwa mijigari kwenda kuserebuka msimu huu wa x mass
 
IMG-20171223-WA0017.jpg
 
Kilimanjaro Noma Sana Yaani Hata Ubungo Stand Wamejaa Safari Kwao
 
Ukidunduliza sh elfu ishirini kila mwezi, kwa miezi kumi na mbili tayari una laki mbili na arobaini! Hapo hujaweza kwenda Moshi na kurudi? Wenzetu huwa wana utaratibu wa ku save hivyo mwisho wa mwaka kujikuta na uwezo wa kwenda kula sikukuu home, wengine na mie tukishika visenti tunatumia mpaka shilingi ya mwisho ndio tutulize 'mishono'...
 
Yao wewe ukiwa unalalamika vyuma vimekaza ndo fursa ya wenzako kutusua, haya wahaya waende nao bukoba mana wanapenda sana battle hawa watu
 
Sisi wachaga hatutumii vyuma tunatumia mbao.

Vyuma vikikaza tunasikia malalamiko kwa wenzetu sisi mwendo wa mbao tu
 
Wataachaje kwendwa wakati mizimu ya mababu na mabibi ipo huko. Mimi mizimu yangu huwa inasafiri na kunifuata popote nilipo kama itv popote. Sihitaji kusafiri kila mwaka.
 
Sio ya mwaka huu hiyo lakini kila mwaka mbona mnaleta hiyo hiyo
Mkuu hata Kama picha ni ya mwaka Jana ila leo nimeshuhudia msusuru wa magari kibao hapa Segera, wachaga noma yaani njia ya Korogwe imejaa magari yanaelekea Moshi unaweza kuhisi kuna msafara wa kiongozi au imekua foleni ya Dsm
 
Wamejipanga sana hawa jamaa aisee..wanasemaga mjini wamekuja kutafuta tu lakini nyumbani ni Moshi. Hii inawafanya kuendelea kuendeleza nyumbani ikiwa ni pamoja na kujenga majumba yakiwemo maghorofa, hamu ya kurudi nyumbani hapo lazima iwepo tu.

Jingine ni kwamba wazee wa kichaga kuhamia kwa watoto wao mjini eti kisa ana Mali hilo kwao ni mwiko, atakuja kwa shughuli maalum au kutibiwa akimaliza anamwambia ngoja nikaangalie kule mgombani kwangu kusije kuharibika mwanangu.
 
Ungepiga ututumie sasa mkuu.sina tatizo na ilo ni kawaida yao hao
 
Hiyo barabara inabomolewa kupisha ujenzi wa SGR (standard gauge Road) , sijui mtapita wapi. bado mna ujeuri!
 
Wamejipanga sana hawa jamaa aisee..wanasemaga mjini wamekuja kutafuta tu lakini nyumbani ni Moshi. Hii inawafanya kuendelea kuendeleza nyumbani ikiwa ni pamoja na kujenga majumba yakiwemo maghorofa, hamu ya kurudi nyumbani hapo lazima iwepo tu.

Jingine ni kwamba wazee wa kichaga kuhamia kwa watoto wao mjini eti kisa ana Mali hilo kwao ni mwiko, atakuja kwa shughuli maalum au kutibiwa akimaliza anamwambia ngoja nikaangalie kule mgombani kwangu kusije kuharibika mwanangu.
Hili ni kweli
 
Vyuma vimekaza kweli, hao wachaga wanaenda kwao kuchua grisi ya kulegeza vyuma
 
Mkuu hata Kama picha ni ya mwaka Jana ila leo nimeshuhudia msusuru wa magari kibao hapa Segera, wachaga noma yaani njia ya Korogwe imejaa magari yanaelekea Moshi unaweza kuhisi kuna msafara wa kiongozi au imekua foleni ya Dsm

ahahaha Wachagga oyooo

demi
 
Back
Top Bottom