Mkuu
Kitoabu, na majibu mazuri ya
King'asti,
measkron ningependa kuongezea kuwa;
Mimba kutoka,
Tatizo hili(kutoka/kuharibika kwa ujauzito) yaanimimba ya wiki 28..hutokana na mambo/vitu mbalimbali vikiwepo.
-Magonjwa ya Kurithi(Autoimmune diseases kama APS)
-Matatizo ya kimaumbile(hasa katika kizazi)
-Madawa (Baadhi ya dawa kutumika katika ujauzito)
-Magonjwa ya zinaa, UTI(infections)
Hayo ni baadhi ya MACHACHE yanayoweza kusababisha mimba kutoka, lakini jambo la muhimu hasa ni kujua mimba/ujauzito ulitoka/kuharibika katika umri gani wa mimba "miezi mingapi"
Mara baada ya mama/mwanamke kushika ujauzito/mimbamabadiliko mbalimbali hutokea ili kusaidia katika ukuaji wa mtoto aliye tumboni(tumbo la uzazi).Hayo huwa katika upumuaji, mfumo wa damu, mfumo wa uzazi n.k.
Hali hii hurudi katika hali yake ya awali taratibu na takribani baada ya mwaka mmoja hali ya mama aliyejifungua(Fiziolojia-yaani utendaji kazi wa mwili) huwa sawa na ya mwanamke yeyote asiye na ujauzito.Hata hivyo baadhi ya wanawake hupoteza ujauzito kabla ya kujifungua..Hii haimaanishi hali ya utendaji kazi wa mwili hurudi papo hapo, na hivyo angalau kwa miezi sita huweza kuvumilika(tolerated).