Hivi wafanyakazi wa TRA mna matatizo gani? Mnaomba omba hela za rushwa kila huduma kwa mteja!

Hivi wafanyakazi wa TRA mna matatizo gani? Mnaomba omba hela za rushwa kila huduma kwa mteja!

Njaaaaa

Hawatosheki na mshahara wao

Kumbuka kila mbuzi anakula kutokana na urefu

Wa kamba yake

Ova
 
Nilichoona TRA hasa kitengo cha kubadilisha umiliki wa Gari, kuna mama pale hafanyi kazi kama hujamuwekea pesa kwenye document zako kupata Control namba ilinichukua massa 7 lakini kuna vishoka wanamuita mama nae anaitika na kuwapa control namba ilibidi niwe Mkali ndipo akanitolea kwa kweli wafanyakazi wa kitengo kile wamejiwekea malengo ya kukusanya pesa za hongo kwa siku na kama kazi haina hongo haifanywi sijui tunaelekea wapi??!! Hebu vyombo husika fuatilieni hapo
Taja tawi gani mkoa gani wilaya gani na hata jina litaje
 
Kama mawaziri wanataka rushwa, viongpzi wa CCM wanataka rushwa, unategemea wafanyakazi wengine wasitake rushwa?

Ofisi za Serikali na mahakama, kote huko ukienda uhakikishe umeandaa hela. Kadiri hela yako inavyozidi kuwa kubwa ndivyo watu watakavyohangaika na kuchacharika kukuhudumia.

CCM ndiyo iliyounda Serikali. CCM hupati nafasi hata ya kwenda kuoigiwa kura bila rushwa. Sasa hivi kwaajili ya kumpata spika wa Bunge, kila mgombea anahangaika kupata hela ya kuwapa wajumbe wa kamati kuu ili jina lake lipitishwe. Sasa huyo jina lake likipitishwa kwa kutoa rushwa, atakataa rushwa?

Tuna cha tawala cha rushwa, kilichounda serikali ya rushwa, iliyojaa watendaji wala rushwa.
 
Hili jambo huwa linakera sana kwamba mtu analipia huduma ambayo ni haki yake kuipata.
 
Back
Top Bottom