Tatizo lipo kwenye lugha, mnalazimisha Kiswahili kwa kila mtu, nakumbuka humu walikua wanakuja Wanijeria na watu wa Afrika Kusini, mada inajadiliwa kwa Kingereza, Watanzania wanajibu jibu humo kwa Kiswahili hadi jamaa wanahisi kama wamebaguliwa.
Mnafaa mjifunze kuwa na uwezo wa kuzungumza lugha kadhaa, sio unadumaa kwenye lugha moja miaka yote, akija mtu wa Ghana unatema yai, akiibuka Mkenya unabadilisha na kutiririka Kiswahili. Ujanja wa lugha ni kitu cha muhimu. Na pia hata sayansi imebaini kwamba watu wenye uwezo wa kuongea lugha zaidi ya moja huongeza akili na maarifa.
Sisi Wakenya tunachangamkia lugha zetu za asili, pia Kiswahili na Kingereza, hapa nyumbani wanangu wanaachia hadi Kifaransa na kuniacha nimedata, ukizingatia pia nimekua nahakikisha wanaongea lugha yangu ya asili yaani Kikikuyu.
Kwenu huko hadi mkulu ameogopa kutoka ndani ya nchi akidai kubana matumizi, ila inafahamika tatizo lipo kwenye lugha maana kule kwa mabeberu bila kutema yai mambo hayaendi. Leo hii hata Wachina na Warusi wote wanahangaika kujifunza Kingereza.