Hivi wahandisi wetu huwa wanawaza nini kuweka vituo vya daladala barabarani?

The Evil Genius

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
6,017
Reaction score
19,506
Kuna vitu unaviona hata kama sio mhandisi lakini unashangaa, huyu ama hawa wahandisi wamesomea wapi?

Ukiangalia barabara zote za Dar kiuhalisia hakuna foleni kiviile ila shida kubwa inayochangia kuwepo na foleni ni vituo vya daladala kua barabarani ama karibu sana na taa za Barabarani.

Mfano, mwenge baada tu ya mataa kituo cha daladala na kiko barabarani, Morocco, Tabata, Buguruni (hiki baadae waliamua kukisogeza mbele kidogo maana kilikua kwenye mataa kabisa), Tazara na kadhalika. Hivyo viko karibu na mataa.

Najiuliza kwa nini wahandisi wetu hawaoni mbali ama hawaoni kabisa kua vituo vya daladala barabarani vitasababisha foleni zisizo na msingi?
 
Plani ni kuondoa daladala jijini zibaki mwendokasi tu
 
Hafu daladala ndo huongeza foleni kwa kusimamisha hata barabarani, daladala zingetakiwa ziwe na njia ya pembeni kabisa kushushia abiria, ka ile barabara ya east Africa arusha hyo ni solution mojawapo
 
Walilelewa na Mwendazake wa kujiita (initials) Eng. XYZ
 
Plani ni kuondoa daladala jijini zibaki mwendokasi tu
shida mambo yanaenda bila utaratibu, usafiri wa tanzania unatakiwa usimamiwe na jiji na sheria za mafisaidi zizingatiwe maana vitu vingi vinafilisika kwasababu tunacheka na wezi wa mali za uma kama uda ilikufa na wezi tunawajua tunawachekea basi tanzania haitakuja kuendelea
 
yani baada ya kuandika hii ndio unawashtua usingizini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…