Hivi waheshimiwa wabunge hamuelewi kama waalimu hatujaaliwa?

Mwamgunda

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
247
Reaction score
48
Nimekuwa nikifatilia mjadala wa bunge tangu kuanza kwake wiki iliyopita, wamejadili na kuuliza mambo mengi kuhusu wizara ya elimu, lakini sijasikia mbunge yeyote akiuliza kuhusu kuajiriwa kwa waalimu mwaka huu wa 2013, sasa najiuliza ina maana wabunge wote mlio bungeni hamuelewi au hamuoni umuhimu wowote kuhusu hili suala kitaifa? Hiyo Mitalaa mnayojadili kila siku itatekelezwa vipi bila kuwepo na waalimu? Nawasilisha.
 
Kama vipi nikupatie namba ya simu ya mulugo umuulize ndo atakata kiu yako ya ajira kama ipo au haitakuwepo kwa mwaka huu.
 
Waalim.. Ah my dia waalim.. Ah .. Inauma..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…